http://www.swahilihub.com/image/view/-/5015362/medRes/2274176/-/jtrrhcz/-/wanaume+pic.jpg

 

Wanawake wenye waume hawa hatarini

 Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watu wazima  Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Dk Delilah Kimambo 

Na  Jackline Masinde, Mwananchi jmasinde@mwananchi.co.tz

Imepakiwa - Friday, March 8  2019 at  13:25

 

Dar es Salaam: Wanawake walioolewa na wanaume wanaovuta sigara, wanywaji wa pombe kali na walio katika kikomo cha hedhi wapo katika hatari zaidi ya kupata magonjwa ya moyo na kiharusi.

Hayo yamesemwa na daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watu wazima kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Dk Delilah Kimambo wakati wa upimaji wa magonjwa ya moyo kwa wanawake kwa lengo la kuhamasisha mazoea ya upimaji afya, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani leo.

Alisema tafiti za hivi karibuni zimeonyesha magonjwa ya moyo na kiharusi yanasababisha vifo kwa wanawake wengi duniani, ambapo mwanamke mmoja katika kila watatu anakufa kwa magonjwa hayo na asilimia 90 wanaviashiria hatarishi vya kuugua.

“Mwanamke anayeishi kwa muda mrefu na mwanamume anayevuta sigara anaweza kupata madhara ya moyo kupitia moshi wa sigara anayovuta mume wake,” alisema.

Dk Delilah alisema mbali na moshi wa sigara, pia mwanamke anapofiki kikomo cha hedhi anakuwa kwenye hatari kupata magonjwa ya moyo.

Mwananchi ilizungumza na baadhi ya wanawake waliofika kupima magonjwa ya moyo ili kujua kama wanafahamu viashiria vya ugonjwa hayo, wengi walisema hawajui.