http://www.swahilihub.com/image/view/-/4929294/medRes/2220376/-/lx9kqsz/-/isack.jpg

 

Wasafirishaji wapinga sheria ya uzito EAC

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe 

Na Khalifa Said, Mwananchi

Imepakiwa - Thursday, January 10  2019 at  14:55

Kwa Muhtasari

Kutumika kwake kutaathiri  uchumi wa nchi kwa jumla

 

ksaid@tz.nationmedia.com

Dar es Salaam. Wafanyabiashara wanaojihusisha na usafirishaji wameilalamikia sheria mpya ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) inayolenga kudhibiti uzito wa mzigo unaopakizwa kwenye magari ya usafirishaji wakisema kutumika kwake si tu kutawaathiri bali pia itaathiri uchumi wa nchi kwa jumla.

Wasafirishaji hao wamesema wameshangazwa na hatua ya Serikali kuruhusu kutumika kwa sheria hiyo huku ikijuwa kwamba baadhi ya vipengele vyake vinapingana na vya sheria zinazosimamiwa na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (Sadc) katika kusimamia ulinzi wa barabara.

Kwa mujibu wa waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano, Isack Kamwelwe wakati akizungumza na kituo cha radio cha Clouds FM jana, sheria hiyo inalenga kutunza barabara za Tanzania ili zisiharibiwe na magari yanayosafirisha mizigo yenye uzito mkubwa.

“Hapa Tanzania kiwango cha mwisho cha mzigo kinachoruhusiwa kubebwa na gari la mzigo na kutembea katika barabara zetu ni tani 56. Kenya wao ni tani 54 wakati Afrika Kusini ni tani 51. Kwa Ulaya ni tani 46,” alisema Kamwelwe.

Sheria hiyo inayojulikana East Africa Community Vehicle Load Control Act, 2016 na kupitishwa mwaka 2017, ambayo inapingwa na wasafirishaji wa mizigo nchini inalenga kuzuia upakiaji wa mizigo kupita kiwango kinachotakiwa katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.