http://www.swahilihub.com/image/view/-/5051194/medRes/2298517/-/rekdl4/-/watanzania+pic.gif

 

Watanzania kuishangilia Serengeti Boys kwa nguvu

Na mwandishi wetu

Imepakiwa - Monday, April 1  2019 at  12:23

 

Machi 12 Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) liliandaa semina kwa makatibu wakuu wa klabu zinazoshiriki mashindano ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Katibu wa klabu ndiye mtendaji mkuu wa shughuli za kila siku za kiundaji, hivyo semina hiyo ilikuwa na manufaa makubwa kwao.

Klabu za Ligi Kuu zililazimika kuajiri katibu mkuu na ofisa habari baada ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kuboresha kanuni zake katika eneo hilo.

Pamoja na Fifa kutoa mwongozo, lakini idadi kubwa ya klabu za Ligi kusimamia kanuni za usimamizi wa soka baada ya kutungwa.

Kwa namna yoyote klabu haziwezi kukwepa kushirikiana na TFF katika usimamizi wa kanuni na sheria husika kwa lengo la kuboresha mchezo wa soka nchini.

Ni wakati mwafaka kwa viongozi wa klabu kujitambua kufahamu wamepewa dhamana ya kuongoza, hivyo ni vyema wakatimiza wajibu wao ili kuleta mabadiliko ya soka.

Ingawa hakuna kanuni au kipengele kinachowabana watendaji hao, lakini nadhani sasa ni wakati mwafaka kwa TFF kuangalia uwezekano wa kutunga kanuni itakayozibana klabu ambazo zitashindwa kutimiza wajibu wao hasa wa kiundaji.

Ni vyema TFF ikachukua hatua dhidi ya klabu ambazo zitakiuka kanuni za usimamizi wa soka ili kupunguza au kukomesha vitendo vya utovu wa nidhamu.