http://www.swahilihub.com/image/view/-/4649182/medRes/2063840/-/12x9cu6z/-/mbar.jpg

Waziri Mbarawa jitofautishe na watangulizi wako

Makame Mbarawa

Waziri wa Maji na Umwagiliaji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Profesa Makame Mbarawa. Picha/MAKTABA  

Na Mwandishi Wetu

Imepakiwa - Friday, July 6  2018 at  09:56

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa ameingia kazini na kutoa maagizo muhimu ambayo kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wanaweza kuyapokea kwa mikono miwili. Akizungumza na wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasco), Profesa Mbarawa amenukuliwa na gazeti hili akiiagiza mamlaka hiyo kuwaunganishia maji wateja 850, 000 ifikapo mwisho wa mwaka huu wa fedha.

Alitoa agizo hilo kwa kile alichosema kutoridhishwa na idadi ndogo ya wateja 290,000 ambayo Dawasco imefikisha, akidai kuwa watu wengi wanahitaji huduma hiyo lakini hawajafikishiwa.

Haya ni maagizo yenye kuleta matumaini, lakini je yatabaki kuwa maagizo na kubaki hivyo kama ilivyozoeleka kwa mipango mingi ya wizara hiyo au tutaona sasa yakiwekwa kwenye utendaji?

Waziri Mbarawa si mtendaji wa kwanza katika sekta ya maji. Mawaziri waliomtangulia wanakumbukwa kwa kutoa kauli tele zenye matumaini kuhusu maji nchini, lakini watendaji wakawaangusha.

Sio Dar es Salaam pekee, kilio cha maji kimeenea kila kona ya nchi pamoja na kuwapo kwa mamlaka nyingi za maji ambazo kimsingi tunaweza kusema zimekuwa mamlaka kwa jina, lakini sio kufikisha maji ipasavyo kwa wananchi.

Mamlaka na taasisi za usimamizi wa maji nchini haziwajibiki ipasavyo katika mgawanyo wa huduma hiyo, kudhibiti uharibifu wa vyanzo vya maji, kupungua na kuisha kwa maji.

Jamii isipokuwa na maji, mambo mengi yanaweza kuibuka ikiwamo uvunjifu wa amani kama tunavyoshuhudia katika maeneo mbalimbali nchini ambako wananchi wamejikuta katika migogoro isiyoisha itokanayo na uhaba wa huduma hiyo katika shughuli zao za uzalishaji.

Waziri Mbarawa ana kazi ya kuhakikisha migogoro ya maji inakoma. Suala hili  linawezekana kwa kuwapo usimamizi na ugawaji mzuri wa rasilimali hiyo ambayo kwa mujibu wa Rais John Magufuli pamoja na kutengewa fedha, watendaji wamekuwa wakimwangusha.

Ifike mahali sasa mipango, maagizo na mikakati ibadilike na kuwa vitendo na hapa ndipo Profesa Mbarawa sio tu atajitofautisha na watangulizi wake, lakini ataacha jina na urithi uliotukuka katika utumishi wake wa umma.

Kutolewa kwake Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi na kwenda kusimamia sekta nyeti ya maji ni dhahiri kwamba Rais amemwamini.

Tunapomkaribisha katika wizara hii yenye changamoto lukuki, lazima atambue kuwa maji ndio uhai wa Taifa letu.

Tunapomtaka kuiweka mipango na mikakati yake katika vitendo, tumkumbushe pia changamoto kadhaa zinazoitesa sekta ya maji nchini ikiwamo kubwa ya usimamizi mbovu wa miradi.

Shughuli zinazohusu matumizi ya maji majumbani, kwenye kilimo, viwanda, uchimbaji wa madini na uzalishaji umeme unategemea usimamizi mzuri wa maji kutoka katika mamlaka zetu ambazo nyingi haziwajibiki ipasavyo.

Tanzania ya viwanda na ya uchumi wa kati ambao Serikali ya Awamu ya Tano inaipigia debe, pamoja na mambo mengine muhimu inahitaji uhakika wa maji kwa wananchi na katika maeneo yote ya uzalishaji.

Hili linawezekana kama Profesa Mbarawa na watendaji wenzake wataweka kwenye vitendo yale yote wanayozungumza kwenye majukwaa.

 Alitoa maagizo hayo kwa kile alichosema kutoridhishwa na idadi ndogo ya wateja 290,000 ambayo Dawasco imefikisha, akidai kuwa watu wengi wanahitaji huduma hiyo lakini hawajafikishiwa.

Haya ni maagizo yenye kuleta matumaini, lakini je yatabaki kuwa maagizo na kubaki hivyo kama ilivyozoeleka kwa mipango mingi ya wizara hiyo au tutaona sasa yakiwekwa kwenye utendaji?

Waziri Mbarawa si mtendaji wa kwanza katika sekta ya maji. Mawaziri waliomtangulia wanakumbukwa kwa kutoa kauli tele zenye matumaini kuhusu maji nchini, lakini watendaji wakawaangusha.

Sio Dar es Salaam pekee, kilio cha maji kimeenea kila kona ya nchi pamoja na kuwapo kwa mamlaka nyingi za maji ambazo kimsingi tunaweza kusema zimekuwa mamlaka kwa jina, lakini sio kufikisha maji ipasavyo kwa wananchi.

Mamlaka na taasisi za usimamizi wa maji nchini haziwajibiki ipasavyo katika mgawanyo wa huduma hiyo, kudhibiti uharibifu wa vyanzo vya maji, kupungua na kuisha kwa maji.

Jamii isipokuwa na maji, mambo mengi yanaweza kuibuka ikiwamo uvunjifu wa amani kama tunavyoshuhudia katika maeneo mbalimbali nchini ambako wananchi wamejikuta katika migogoro isiyoisha itokanayo na uhaba wa huduma hiyo katika shughuli zao za uzalishaji.

Kwa kuwa ameanza na Dawasco, tunatarajia kuwa moto aliouwasha hapo utasambaa katika mamlaka nyingine zote nchini.

 Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa ameingia kazini na kutoa maagizo muhimu ambayo kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wanaweza kuyapokea kwa mikono miwili. Akizungumza na wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasco), Profesa Mbarawa amenukuliwa na gazeti hili akiiagiza mamlaka hiyo kuwaunganishia maji wateja 850, 000 ifikapo mwisho wa mwaka huu wa fedha.

 Jamii isipokuwa na maji, mambo mengi yanaweza kuibuka ikiwamo uvunjifu wa amani kama tunavyoshuhudia katika maeneo mbalimbali nchini ambako wananchi wamejikuta katika migogoro isiyoisha itokanayo na uhaba wa huduma hiyo katika shughuli zao za uzalishaji.

 Kutolewa kwake Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi na kwenda kusimamia sekta nyeti ya maji ni dhahiri kwamba Rais amemwamini.

Na tunapomkaribisha katika wizara hii yenye changamoto lukuki, lazima atambue kuwa maji ndio uhai wa Taifa letu.