http://www.swahilihub.com/image/view/-/2944250/medRes/1168167/-/13wi3ts/-/wema.jpg

 

Wema Sepetu pia awabana wafuasi wake mtandaoni

Wema Sepetu

Mwigizaji wa filamu za Bongo Wema Sepetu. Picha/HISANI 

Na PAULINE ONGAJI

Imepakiwa - Thursday, January 5  2017 at  16:27

Kwa Mukhtasari

YAONEKANA kana kwamba sasa umekuwa mtindo kwa watu maarufu kuondoa maelezo kujihusu kutoka mitandao ya kijamii.

 

Zamu hii ilikuwa ya muigizaji na mwanasosholaiti mzaliwa wa Tanzania Wema Sepetu.

Japo hakuchukua hatua ya kuzima kabisa akaunti yake ya Instagram, muigizaji huyo anaaminika kuzima kila kitu kwenye akaunti yake ya mtandao huo wa kijamii bila kutoa sababu ya hatua yake.

Baadhi ya wakosoaji wake wanahoji kuwa huenda anajiandaa kuanza mwaka mpya bila utata.

Mwaka 2016 mwanasosholaiti huyu ambaye wakati mmoja alikuwa mpenzi wa nyota wa muziki, Diamond, aliibua utata mara kadha huku kashfa yake ya hivi majuzi ikimhusisha na uhusiano wa mapenzi na mwanamitindo kwa jina Kalisa ambapo video ya wawili hao wakibusiana hadharani ikichipuka.