Wendy William na wanawake wanaowaibia wanaume wa watu

Imepakiwa - Wednesday, May 15  2019 at  13:44

 

Mtangazaji Wendy William amesema wanawake wenye uhusiano wa kimapenzi na wanaume waliooa ‘watachomwa kwa moto maalumu’ siku ya mwisho.

Wakati akieleza ishu ya mke wa Stephe Curry, Ayesha mtangazaji huyo alikandamizia kwa kusema wapo wanawake wengi wasioheshimu ndoa za watu.

Ayesha ambaye ni mke wa mcheza kikapu huyo maarufu alisema mume wake amekuwa akipata usumbufu kutoka kwa wanawake na wakati mwingine hata akiwa naye.

“Kuna mwanamke alifungua gari letu na moja kwa moja akajisogeza kwa mume wangu akitaka wapige picha, nilimwangalia tu,” alisema Ayesha.

Wendy yupo katika harakati za kutalikiana na mumewe, Kevin Hunter baada ya ndoa yao ya miaka 22 kuingiliwa na mdudu wa usaliti.

Inadaiwa kuwa Hunter ambaye alikuwa meneja wake, amekuwa akimsaliti Wendy na amepata mtoto katika nyumba ndogo.