http://www.swahilihub.com/image/view/-/3795570/medRes/1551023/-/fkrpnf/-/ya.jpg

 

Wolper, Harmonize moto umewaka

Jacqueline Wolper

Mrembo mwigizaji Jacqueline Wolper. Picha/HISANI 

Na MWANASPOTI

Imepakiwa - Thursday, May 10  2018 at  15:20

Kwa Muhtasari

  • Wolper na Harmonize wametupiana maneno makali ya vijembe katika kurasa zao za mtandao wa Instagram baada ya habari kuvuja zikidai yule demu Mzungu wa Harmonize anayeitwa Sarah, amemtosa na kumchukua baunsa wa Diamond Platnumz anayejulikana kwa jina la Mwarabu Fighter.
  • Kwenye mahojiano Wolper anasema anajua Mwanaspoti inataka kuuliza nini na kwamba yeye hataki kumzungumzia Rajabu (Harmonize), "achana naye bwana, maana tutaendelea kumpa kiki zisizokuwa na maana, we njoo dukani kwangu tufanye mahojiano ya kazi zangu rafiki".

 

SIKU mbili zilizopita, kumeibuka mtafaruku baina ya wapenzi wa zamani, staa wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper na mwanamuziki Harmonize.

Wolper na Harmonize wametupiana maneno makali ya vijembe katika kurasa zao za mtandao wa Instagram baada ya habari kuvuja zikidai yule demu Mzungu wa Harmonize anayeitwa Sarah, amemtosa na kumchukua baunsa wa Diamond Platnumz anayejulikana kwa jina la Mwarabu Fighter.
Habari zinadai kuwa Sarah amezimika kwa Mwarabu Fighter hadi kufikia hatua ya kumpangishia nyumba na huduma zote alizokuwa anapata Harmonize sasa amezihamishia kwa Mlinzi huyo wa Diamond. Sarah na Wolper wamekuwa kwenye vita ya mapenzi huku ikidaiwa chanzo ni penzi la Harmonize, lakini baada ya tetesi hizo za usaliti kusambaa mitandaoni, mtangazaji wa kituo kimoja cha Televisheni alimsaka Wolper na kumuuliza nini maoni yake juu ya ishu hiyo na ndipo timbwili lilipoanza.
Katika mazungumzo hayo, Wolper alimtupia dongo zito Sarah, na kujibu hivi:

“Duh hiyo ishu mbona ni exclusive (ya kipekee) kabisa sijaisikia lakini ni freshi tu. Mbona yule demu (Sarah) ni mlezi wa wana, labda kachoka kumlea huyu kaamua kumchukua mwana mwingine, freshi tu”.

Baada ya kipande cha video ya mahojiano ya Wolper kusambaa katika mitandao ya kijamii, Hamornize alimtetea Mzungu wake kwa kumjibu Wolper kupitia akaunti yake ya Instagram.

Nyota huyo kutoka kampuni ya WCB inayomilikiwa na Diamond Platnumz, aliwaorodhesha wanaume ambao Wolper amewahi kutoka nao kimapenzi na kudai kuwa Sarah sio mlezi wa wana bali Wolper ndiye mlezi wa wana.

Hapo ndipo gazeti la Mwanaspoti liliamua kumtafuta Wolper na kufanya naye mahojiano.

Mwanaspoti: Habari yako Wolper?

Wolper: Nzuri tu Rhobi, najua unataka uniulize nini, mie kwa sasa sitaki kumzungumzia Rajabu (Harmonize), achana naye bwana, maana tutaendelea kumpa kiki zisizokuwa na maana, we njoo dukani kwangu tufanye mahojiano ya kazi zangu rafiki.

Mwanaspoti: Mbona umeniwahi, umejuaje kama nataka kukuuliza habari za Harmonize (Rajabu)? Pengine nataka kukwambia kitu kingine.

Wolper: Ahh! wapi, wewe au mtu mwingine? Huwa unaniua kama hunijui mdogo wako na isitoshe kwa tukio la jana utaachaje kuniuliza hilo swali, haya uliza nina dakika kama tano hivi za kuongea na wewe.

Mwanaspoti: Sawa, nianzie hapo hapo, hivi kwanini katika mahojiano yako, ukiulizwa swali la Harmonize au Sarah huwa unajibu vibaya sana?

Wolper: Sababu huwa sipendi kuwazungumzia hao watu na huwa nalazimishwa kujibu kutokana na swali. Unajua mtu kama hutaki kitu basi unajibu tu ili kuwakera japo huwa najiona nipo sahihi katika majibu yangu.

Mwanaspoti: Watu wanadai wewe na Harmonize bado mnapendana, wengine husema ni wapenzi wa kimya kimya na ndiyo maana mnafuatiliana sana katika posti zenu katika mitandao ya kijamii na hata katika mahojiano hamuachi kutajana. Hili lina ukweli?

Wolper: Sikia nikwambie, mimi na Rajabu (Harmonize) kwanza hatujawahi kutamkiana kuwa tumeachana, pia siwezi kumfuatilia mtu ambaye unaona kabisa ana mpenzi wake jamani na isitoshe mimi huwa simtaji bali waandishi ndio wanaosababisha nimtaje kutokana na maswali yao.

Mwanaspoti: Huoni ni sababu mojawapo inayoweza kuwafanya wewe na Harmonize kuendelea kutamaniana, kutokana na ukweli kwamba hamjawahi kutamkiana kuwa mmeachana?

Wolper: Hapana. Hiyo siyo sababu bwana, kama mtu kusoma unashindwa hata picha unashindwa kuangalia? Dalili zilikuwa zinaonekana wazi, ndiyo maana mie nikaamua kukaa kimya, naye akanielewa akaendeleza ukimya hadi hapo alipoibuka hadharani kumtambulisha huyo mwanamke wake.

Mwanaspoti: We unadhani kwanini Harmonize aliamua kuwa na Sarah na kukuacha wewe?

Wolper: Harmonize hajaniacha, kwanza uelewe hilo, ila ninachojua kwa kuwa mimi ni maskini na Sarah ni tajiri. Aliniambia kuwa kwa Sarah anafuata pesa hivyo nitulie tu halafu atarudi, sikukubaliana na hilo.

Mwanaspoti: Harmonize aliandika katika Instagram, orodha ya wanaume uliowahi kutoka nao kimapenzi, umelichukuliaje hili suala?

Wolper: Hahaha! Mie nimefurahi tu, tena naona kama ile list (orodha) ni ndogo na wapo wanaume wengine aliowataja sijawahi kujihusisha nao kimapenzi, ila kawaacha wahusika. Ila sema nini? Kiki ni mbaya sana na ndiyo maana nakwambia mimi nikiamua kutaja mambo ya Harmonize nitazidi kumpa kiki tu, bora ninyamaze na kufanya shughuli zangu.

Mwanaspoti: Ikitokea Harmonize amekuja kukuomba msamaha ili mrudiane, uko tayari?

Wolper: Hapana, kwaheri buana.