http://www.swahilihub.com/image/view/-/3815592/medRes/1565535/-/w7wnw5/-/refa.jpg

 

Zippy atoa mafunzo ya kwata kupitia ReInvent You

Zippy Kimani

Bi Zippy Kimani, mwanzilishi wa ReInvent You, shirika linalosaidia waume kwa wanawake walio na matatizo ya uzani, kurejelea hali yao ya kawaida na kujithamini. 

Na PAULINE ONGAJI

Imepakiwa - Thursday, February 16  2017 at  14:49

Kwa Mukhtasari

Kutana na Bi Zippy Kimani, mwanzilishi wa ReInvent You, shirika linalosaidia waume kwa wanawake walio na matatizo ya uzani, kurejelea hali yao ya kawaida na kujithamini.

 

KWA miaka miwili sasa amekuwa akisaidia watu na hasa wanawake kujithamini kupitia mazoezi.

Kutana na Bi Zippy Kimani, mwanzilishi wa ReInvent You, shirika linalosaidia waume kwa wanawake walio na matatizo ya uzani, kurejelea hali yao ya kawaida na kujithamini.

Shirika hili limeunganisha vikao vya mazoezi na ushauri hasa kwa watu ambao hawajithamini tena baada ya miaka ya kukejeliwa kwa sababu ya uzani wao.

Kwa sasa wana mpango wa watu binafsi ambapo tangu mradi huu uanzishwe wamesaidia zaidi ya watu 100 kuafikia malengo yao hasa katika suala la uzani.

Anasema alikuwa na ndoto ya kuanzisha mpango wa mazoezi tangu utotoni; anasema alipopoteza ajira ndipo alijitolea kikamilifu na kuamua kutumia jukwaa hili kama kitega uchumi.

Bi Kimani hajihusishi tu na masuala ya mazoezi kwani yeye pia ni mshauri wa vijana, huduma ambayo amekuwa akitoa kwa miaka miwili sasa.

Anafanya haya kwa ushirikiano na mashirika kama vile The League of Young Professionals, Akad Educational Group na Precious Sisters ambapo wametembelea shule za upili kama vile Starehe Girls, Moi High School Kabarak na Precious Blood Riruta miongoni mwa zingine.

Kwa kawaida wao hutembelea shule hizi kila muhula ambapo huchagua watoto kutoka familia maskini ambapo jukumu lao ni kufuatilia masomo yao na kuhakikisha kuwa wanafanya vyema.

Maisha

Azma yake ya kujihusisha na masuala haya ya ushauri yanatokana na maisha aliyopitia ambapo matatizo ya kifedha yalimfanya kukosa karo.

Ni suala lililoathiri matokeo yake katika mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne ambapo alipata alama ya C, kumaanisha kuwa hakupata nafasi ya kujiunga na chuo kikuu.

Hata hivyo hakufa matumaini na jaribio lake la pili kufanya mtihani wa kidato cha nne lilizaa matunda ambapo alipata alama ya B+ na kujiunga na chuo kikuu na kusomea sheria.

Mbali na hayo anafanya kazi na Out of the Streets Foundation kushauri vijana wa mtaani ambapo lengo lake ni kuwasaidia wasihisi kana kwamba eti kwa sababu wanaishi maisha magumu basi hawawezi afikia ndoto zao maishani