http://www.swahilihub.com/image/view/-/4560220/medRes/1971966/-/2sp9d1/-/igiza.jpg

 

Amepania kumfikia veterani Patience Ozokwor 

Jerusah Atemo Mane

Mwigizaji Jerusah Atemo Mane. Picha/ Picha/JOHN KIMWERE 

Na JOHN KIMWERE

Imepakiwa - Monday, May 14  2018 at  07:43

Kwa Muhtasari

  • Mrembo Jerusah Atemo Mane 33, anasema anatamani sana kuibuka mwigizaji wa haiba kubwa duniani.
  • Anataka kuwa staa kimataifa kama mwigizaji, mwimbaji, mwana mitindo na dezaina shupavu nchini Nigeria Patience Ozokwor maarufu Mama G. 

 

LISEMWALO lipo, kama halipo laja. Kenya ni taifa tajiri kupindukia katika sekta ya sanaa, maana wapo chipukizi wengi tu wanawake na wanaume waliokirimiwa kipaji cha muziki pia maigizo, lakini kutokana na sababu mbali mbali hawajafaulu kutambulika wangali chini ya maji.

Katika muziki hali ya hukosefu wa fedha kuwapiga jeki kujiendeleza hasa kutoa kazi nzuri kiasi inawaponda wanamuziki wanaoibukia.  Nayo sanaa ya maigizo imekosa sapoti huku serikali ikipuuzilia mbali sekta ya filamu na kufanya wengi wao kukosa nafasi mwafaka ya kujikuza baada ya jitihada zao kuambulia patubu.

Dada Jerusah Atemo Mane 33,  ni kati ya waigizaji wa kike wanaokuja hapa nchini licha ya kujituma mithili ya mchwa.

Binti huyu anayejivunia kuonja matunda ya kushiriki baadhi ya movie za humu nchini anasema ana uwezo tosha kufanya vizuri na kuibuka mahiri kama wenzake katika mataifa ya Ghana, Nigeria na Tanzania kati ya mengine. 

Hakika sio mgeni kwa wapenda filamu nchini baada ya kubahatika kushiriki muvi mbai mbali zilizorushwa katika vituo vya televisheni ikiwamo NTV na Maisha Magic. Mwaka 2015 alikuwa miongoni mwa waliohusika kutengeneza filamu zilizorushwa na NTV kipindi cha  'Visanga' (comedy series 1-7). 

Ni kati ya vipindi vilivyokuwa vikitengenezwa na kampuni ya Cinematic Solution.

Baadaye alifanya kazi na Spieldwork Media walikotengeneza filamu kadhaa zilizofanikiwa kurushwa kupitia Maisha Magic kama 'Urembo Saloon,' 'Maisha Njia Panda' akifahamika kama 'Mama wa Chama', 'Shika patapotea 'Rehema,' na Mchungaji 'Saida'.

Mapema Aprili 2018, Atemo Mane alishiriki tangazo la Viusasa linalotazamiwa kukurushwa katika kituo cha Citizen TV kwa lugha ya Kiluhya.

Dada huyu anasema anatamani sana kuibuka mwigizaji wa haiba kubwa duniani. Anataka kuwa staa kimataifa kama mwigizaji, mwimbaji, mwana mitindo na dezaina shupavu nchini Nigeria Patience Ozokwor maarufu Mama G. 

Veterani huyo aliyewahi kufanya kazi kwenye redio stesheni tofauti nchini humo ameshiriki filamu chungu nzima kama 'Blood Sister 2003,' '2 Rats 2003,'  'The wedding party2 2017,' 'Marcus D Milionaire,' 'Code of silence 2015,' 'Abuja top Ladies,' 'Turning point 2012,' na 'The End is near 2012,' kati ya zingine. Aidha kwa wanamaigizo mahiri nchini humo hupenda kuketi na kutazama kazi za waigizaji wengine kama Ini Edo na Mercy Jonson.

Ghana

Kwa Waghana huvutiwa na filamu za waigizaji mahiri Nadiah Buari na Jackie Agyemang Appiah miongoni mwa wengine. Jackie anajivunia kutwaa tuzo ya Best Actress in a leading role at the 2010 Africa movie Academy Awards pia Best actress in a supporting role at the africa movie Academy Awards. 

Pia Atemo aliwahi kufanya kazi na Tripple Adge na Citty Model, alikoshiriki shoo ya kutumia dettol kufanya usafi pia kushiriki matangazo tofauti ikiwamo Jambojet mtawalia.  

Atemo Mane anatazamia kufunga pingu za maisha na mpenzi wake ambaye wamejaliwa mtoto mmoja wa kiume. Aidha anasema amekuwa akiandika mistari ya nyimbo za injili ambazo akipata mtaji aamepania kuelekea studio kuzirekodi na kuanza uimbaji maana amekuwa akiziandika na kuzihifadhi. 

Hata hivyo, siyo mchoyo wa mawaidha anahimiza waigizaji wa kike kutokubali kushushwa hadhi na maprodyuza ambao hutawaka kimapenzi ili kuwapa ajira kuigiza kwenye filamu zao. Kadhalika anawaambia kuwa nyakati zote katika kazi ya maigizo wamapaswa kuifanya kwa kujitolea, kujiamini, kujiheshimu wala wasiwe wenye pupa kwa kuzingatia subira yavuta heri.