http://www.swahilihub.com/image/view/-/3406262/medRes/1453352/-/d2n00mz/-/saida.jpg

 

Ijumaa ya burudani aali kutoka kwa Saida Karoli

Saida Karoli

Mwanamuziki wa nyimbo za kitamaduni nchini Tanzania, Saida Karoli. Picha/HISANI 

Na JOHN ASHIHUNDU

Imepakiwa - Friday, December 7  2018 at  15:11

Kwa Muhtasari

Saida Karoli ni maarufu sana kwa nyimbo za kiasili.

 

NAIROBI, Kenya

MWANAMUZIKI maarufu wa muziki wa kiasili Saida Karoli, Ijumaa jioni anatumbuiza mashabiki katika Club Meladine eneo la Upper Hill, Nairobi kabla ya kuelekea Kaunti ya Kisumu juma lijalo kuwapa burudani mashabiki katika ukumbi wa Tom Mboya Labour College, Ijumaa, Desemba 14, 2018.

Jukwaani, Saida anayetambulika kutokana na wimbo wake wa “Maria Salome”,  atashirikiana na msanii kutoka Jamhuri ya Congo, L. Rice aliyekuwa muimbaji maarufu katika bendi la Ferre Gola na Mkenya Musa Jakadala anayefahamika kwa muziki aina ya Ohangla.

Saida aliwasili katika uwanja wa ndege wa Wilson mapema juma hili akiandamana na mwanamuziki Mkenya Atomy Sifa, ambaye pia amerekodi naye nyimbo kadhaa.

“Ni miaka mingi tangu nitumbuize mashabiki wangu nchini Kenya na nimerejea huku nikiwaahidi makubwa mbali na kuwafurahisha kwa nyimboa kadhaa mpya,“ alisema.

Saida ambaye wimbo wake wa “Maria Salome’ umewahi kurudiwa na wanamuziki kadhaa akiwemo staa Diamond Platnumz, amefika nchini na zaidi ya wanenguaji 10 kwa ajili ya shoo zake mbili.

Miongoni mwa vibaoa vyake matata ni 'Kaisiki', 'Orugambo’ na “Folo’.