http://www.swahilihub.com/image/view/-/4842408/medRes/2164208/-/73tolx/-/cookies.jpg

 

MAPISHI: Cookies

Cookies

Cookies. Picha/MARGARET MAINA 

Na MARGARET MAINA

Imepakiwa - Thursday, November 8  2018 at  12:48

Kwa Muhtasari

Cookies ni biskuti zenye sukari nyingi na ambazo hupendeza sana.

 


MAPISHI: Cookies

Muda wa kuandaa: Dakika 20

Mapishi: Dakika 30

Walaji: 4

Vinavyohitajika 

  • Unga wa ngano kikombe kimoja na nusu.

  • Siagi vijiko 4
  • Sukari vijiko 6
  • Yai 1
  • Vanilla extract
  • Baking soda kijiko kidogo

Maelekezo

Weka Siagi kwenye bakuli lako la kukandia.

Weka sukari na uanze kuchanganya kwa kijiko/mwiko hadi vichanganyike kabisa.

Pasulia yai humo na uchanganye hadi uwe laini na utoe mapovu.

Ongeza unga na uchanganye hadi vichanganyike kabisa.

Weka flavour yako kama vanilla au yoyote ile uipendayo.

Ukishachanganya kila kitu weka kwenye jokovu kwa muda wa nusu saa.

Washa ovena kwenye nyuzijoto 150 Degrees Celcius.

Toa unga kutoka kwenye jirafu.

Changanya unga wako kwa mkono kisha usukume kwenye kibao na ukate shepu mbalimbali.

Panga shepu zako ulizokata kwenye chombo cha kuokea.

Oka cookies zako kwa muda wa dakika 25-30.

Toa cookies zako, ziache zipoe.

Pakua na ufurahie - mimi huzila huku nikiteremsha ama maziwa, juisi,chai au kinywaji chochote nikipendacho kutegemea upatikanaji.