http://www.swahilihub.com/image/view/-/4602062/medRes/2001563/-/8od1pmz/-/yai.jpg

 

Faida za kiafya anazopata mlaji wa mayai

Mayai

Mayai. Picha/HISANI 

Na MARGARET MAINA

Imepakiwa - Thursday, November 8  2018 at  10:09

Kwa Muhtasari

  • Mlaji wa mayai anapata faida nyingi tu
  • Katika makala ya awali niliwahi kuzungumzia faida za mayai katika ulainishaji wa ngozi

 

MAYAI yana faida kadhaa katika mwili wa binadamu.

Miongoni mwa faida hizo ni:

Hutunza shibe

Protini zilizoko ndani ya mayai hukufanya kutohisi njaa mapema. Ina maana kuwa ukila mayai unaweza kukaa muda marefu zaidi bila kula ikilinganishwa na mikate au vyakula vingine vya ngano.

Husaidia kupunguza uzito

Ulaji wa mayai husadia kupunguza uzito wa mwili. Watu wanaokula mayai wamefanikiwa kupunguza uzito wa miili yao kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na wasiokula.

Mayai hupatikana kwa bei rahisi

Ukilinganisha na vyakula vingine vya protini kama vile nyama, mayai ni bei rahisi. Hivyo basi, mayai yanaweza kupatikana na kuandaliwa kwa urahisi wakati wa kifungua kinywa kuliko vyakula vingine.

Mayai ni chanzo kikubwa cha protini

Mayai yana kiasi kikubwa cha protini kinachohitajika katika kujenga miili yetu. Ni vyema kula mayai asubuhi wakati wa kifungua kinywa ili kujipatia virutubisho hivi.

Mayai hayaongezi Cholesterol

Cholestrol iliyoko katika mayai inapoliwa haina athari kwenye mwili.

Husaidia ukuaji wa ubongo na uwezo wa kumbukumbu

Kirutubisho kinachojulikana kama “Choline” kinachopatikana kwenye mayai ni muhimu katika ukuaji wa ubongo. Pia kinahusishwa katika kuongeza uwezo wa ubongo wa kutunza kumbukumbu.

Hulinda macho

Kemikali za leutin na zeaxanthin zinazopatikana kwenye mayai zinaaminika kulinda macho dhidi ya madhara.