http://www.swahilihub.com/image/view/-/2880442/medRes/1125761/-/f5poffz/-/790983-01-02.jpg

 

Faida za kimwili na kiroho za ibada ya Hija

Kaaba

Mahujaji wa Kiislamu wagusa eneo la ibada takatifu, maarufu kama Kaaba, katika msikiti mkuu wa Mecca, Saudi Arabia Septemba 21, 2015. Picha/AFP 

Na HAWA ALI

Imepakiwa - Friday, August 10  2018 at  12:29

Kwa Muhtasari

Ibada hii inalenga kuwakumbusha Waislamu historia ya harakati za Kiislamu zilizoanzia Mjini Makka na kufikia kilele chake cha mafanikio Mjini Madina.

 

Msimu mwingine wa Ibada ya Hijja umewadia.

Tayari Mahujaji kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Kenya wameshaanza kumiminika Mjini Maka.

Tunachukua fursa hii kuwaombea kheri nyingi Mahujaji wote.


Aidha tunatumia nafasi hii kukumbushia mambo ambayo tunaamini viongozi wa Misafara watayasisitiza katika hatua mbalimbali za Ibada hiyo tukufu.


Kabla ya kuondoka kwenda Madina, ni vizuri kuyasoma na kuyakumbuka mambo kadhaa ambayo yatawasaidia Mahujaji kujizidishia fadhila za Hija.

Kwa sura yake ya ndani nguzo hii ya tano ya Uislamu imekusudiwa kuwajenga Waislamu kiroho kupitia ibada katika maeneo mbalimbali
 Mbali ya matendo makuu ya Ibada hiyo, inasisitizwa kwa wale wanaoitembelea Madina kwamba wazuru Masjid Qubaa na kuswali katika Msikiti huo.

Hii imesimuliwa katika Hadith chache kutoka kwa Mtume, swallallahu alayhi wa sallam.
 Abdulla ibn Umar kasimulia kuwa Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, alikuwa akizuru Masjid Qubaa na kuswali humo rakaa mbili. Pia, Sahl ibn Haniif kasimulia kuwa, Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, amesema,
 “Yeyote atiaye udhu nyumbani kwake kisha akaenda Masjid Qubaa na kuswali humo, atapata malipo sawa na yale ya kufanya Umra.” (Ahmad na Nasa’ii).


Halikadhalika ni Sunna kuzuru makaburi ya al-Baqi. Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, alikuwa akizuru makaburi ya al-Baqi na kuwaombea dua wale waliozikwa hapo. Alikuwa akiwaambia Maswahaba zake, “Zuruni Makaburini, kwani yanakukumbusheni Akhera,” (Muslim).Aidha aliwafundisha kusoma dua ifuatayo wakati wa kuzuru makaburini: “Assalamu alaikum ahlad Diyari minal muuminiin wal muslimiin, wa inna inshaAllahu bikum lahiqun. Nas’alullah lana wa lakumul aafiyah,”
 Tafsiri yake, “Enyi wakaazi wa mahali hapa, waumini na Waislamu, Assalaam alaykum. InshaAllah, nasi tunakaribia kukutana nanyi.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu atujaalie sisi na nyie amani na usalama.”
 Kuzuru makaburi kunatukumbusha Akhera. Pia kunatupa fursa ya kuwasaidia wafu ambao hawawezi tena kujisaidia, hii ni kwa kuwaombea rehema na maghfira.


Hili ndilo angalau tunaloweza kulifanya kwao hasa hasa kama wafu hao ni miongoni mwa Waislamu wema na wachaMungu ambao walifanya kazi kubwa ya kuitumikia dini yetu.


Kwa upande wa falsafa ya kimwili ya Hija. Ibada hii inalenga kuwakumbusha Waislamu historia ya harakati za Kiislamu zilizoanzia Mjini Maka na kufikia kilele chake cha mafanikio Mjini Madina.
 Ni ibada inayoamsha ari ya kujitoa kwa hali na mali kwa ajili ya dini ya Mwenyezi Mungu.

Ni safari ndefu ya gharama ambayo inaakisi utayari wa kujitoa kwa ajili ya dini ya Mwenyezi Mungu.

Utiifu

Hija ni shughuli ya kimwili inayotokana na imani ya Hujaji kwamba hakuna chochote chenye thamani katika dunia hii kama utiifu kwa Muumba. Mithili ya askari waliojumuika pamoja baada ya kutii amri ya Kiongozi, mkusanyiko wa Mahujaji Maka ni ishara ya utii kwa Mwenyezi Mungu, na Mtume wake, swallallahu alayhi wa sallam.Ni mkusanyiko wa aina yake unaotimiza dhana ya Umma mmoja bila kujali tofauti za rangi, kipato, elimu, jinsia na kadhalika. Kama kila Hujaji atahiji kwa mazingatio basi inaweza kujengeka nidhamu ya hali ya juu baada ya Ibada hiyo ambapo kila mtu atabadili maisha yake na kuishi kwa utii kama alivyoonesha utii katika hatua zote za ibada hiyo.Matendo yote ya kiroho na matendo yote ya kimwili katika ibada ya Hija yanalenga kuuandaa Umma wa Waumini Duniani kwa mapinduzi ya kiroho na kimwili ili ulimwengu uhame kutoka maisha ya kutenganisha mwili na roho ambayo yameleta janga kubwa la kimaadili na kijamii duniani kote.Kuiacha roho pekee yake bila mwili hakutimizi hitajio la UchaMungu kwani utawa pekee hauwezi kuijenga dunia. Na kuuacha mwili pekee bila roho hakutimizi hitajio la kimaadili ambalo ndilo linalouchunga mwili katika kila nukta ya maishaKwa kuizingatia Ibada ya Hijja, kila Hujaji atakuwa amejenga maisha ya uwiano wa roho na mwili katika kuzikabili changamoto za maisha ya dunia kwa ufanisi. Ibada ya hija inaakisi kisimamo cha Siku ya Kiama ambacho kitakuwa cha kiroho na kimwili.Kwa sababu hiyo, maisha ya roho na mwili ya kila mwanadamu lazima yasalimishwe kwa Mfalme wa Siku ya Mwisho kama yanavyosalimishwa katika ibada ya Hija.
aislamu wema na wachaMungu ambao walifanya kazi kubwa ya kuitumikia dini yetu.Kwa upande wa falsafa ya kimwili ya Hija.

Ibada hii inalenga kuwakumbusha Waislamu historia ya harakati za Kiislamu zilizoanzia Mjini Makka na kufikia kilele chake cha mafanikio Mjini Madina.

Ni ibada inayoamsha ari ya kujitoa kwa hali na mali kwa ajili ya dini ya Mwenyezi Mungu.

Ni safari ndefu ya gharama ambayo inaakisi utayari wa kujitoa kwa ajili ya dini ya Mwenyezi Mungu.Hija ni zoezi la kimwili linalotokana na imani ya Hujaji kwamba hakuna chochote chenye thamani katika dunia hii kama utii kwa Muumba.

Mithili ya askari waliojumuika pamoja baada ya kutii amri ya Kiongozi, mkusanyiko wa Mahujaji Maka ni ishara ya utii kwa Mwenyezi Mungu, na Mtume wake, swallallahu alayhi wa sallam.

Ni mkusanyiko wa aina yake unaotimiza dhana ya Umma mmoja bila kujali tofauti za rangi, kipato, elimu, jinsia na kadhalika.

Kama kila Hujaji atahiji kwa mazingatio basi inaweza kujengeka nidhamu ya hali ya juu baada ya Ibada hiyo ambapo kila mtu atabadili maisha yake na kuishi kwa utii kama alivyoonesha utii katika hatua zote za ibada hiyo.Matendo yote ya kiroho na matendo yote ya kimwili katika ibada ya Hija yanalenga kuuandaa Umma wa Waumini Duniani kwa mapinduzi ya kiroho na kimwili ili ulimwengu uhame kutoka maisha ya kutenganisha mwili na roho ambayo yameleta janga kubwa la kimaadili na kijamii duniani kote.Kuiacha roho pekee yake bila mwili hakutimizi hitajio la UchaMungu kwani utawa pekee hauwezi kuijenga dunia. Na kuuacha mwili pekee bila roho hakutimizi hitajio la kimaadili ambalo ndilo linalouchunga mwili katika kila nukta ya maishaKwa kuizingatia Ibada ya Hijja, kila Hujaji atakuwa amejenga maisha ya uwiano wa roho na mwili katika kuzikabili changamoto za maisha ya dunia kwa ufanisi. Ibada ya hija inaakisi kisimamo cha Siku ya Kiama ambacho kitakuwa cha kiroho na kimwili.Kwa sababu hiyo, maisha ya roho na mwili ya kila mwanadamu lazima yasalimishwe kwa Mfalme wa Siku ya Mwisho kama yanavyosalimishwa katika ibada ya Hija.