http://www.swahilihub.com/image/view/-/4844242/medRes/2165338/-/aqlrx5/-/tikitimaji.jpg

 

Juisi ya tikitimaji

Tikitimaji

Tikitimaji. Picha/MARGARET MAINA 

Na MARGARET MAINA

Imepakiwa - Friday, November 9  2018 at  14:12

Kwa Muhtasari

Juisi ya tikitimaji ni tamu sana.

 

Juisi ya tikitimaji

Muda wa kuandaa: dakika 10

Wanywaji: 2

Tikitimaji ni tunda zuri sana lenye maji mengi na hufaa sana kuliwa wakati wa joto kali hasa linapokuwa lenyewe ni baridi, huburudisha sana.

Amino acid inayopatikana katika juisi ya tikitimaji husaidia mishipa ya damu na kuifanya damu izunguke vizuru sehemu mbalimbal za mwili.

Katika tikitimaji kuna vitamini C, carotene, potassium na magnesium.

Unywaji wa juisi ya tikiti husaidia kwa kiasi kikubwa katika usafishaji wa ammonia na uric acid.

Pia husaidia katika uondoshwaji wa mawe katika figo (kidney stones).

Vinavyohitajika

  • Tikitimaji kubwa

  • Sukari (ukipenda)

  • Ice cubes

Maelekezo

Osha vizuri tunda lako kisha ulikate vipande kama vinane kwa urefu (longitudinally).

Chukua kipande kimoja kimoja na uondoe ganda la nje. Katakata vipande vidogo vidogo na kutoa mbegu kisha weka kwenye blenda.

Saga hadi vilainike kabisa kisha chuja na weka kwenye jagi (weka sukari kama ukipenda)

Juisi iko tayari kwa kunywiwa.

Unaweza kuchanganya juisi ya tikitimaji na ya embe ukitaka uonje utamu wa hali ya juu.