http://www.swahilihub.com/image/view/-/3851982/medRes/1590151/-/118n57xz/-/doga.jpg

 

Kichuna wa CR7 aliwahi kuwa yaya

Cristiano Ronaldo

Cristiano Ronaldo, mpenziwe Georgina Rodriguez na mwana wa CR7. Picha/HISANI 

Na THOMAS MATIKO

Imepakiwa - Thursday, March 16  2017 at  12:45

Kwa Mukhtasari

Kumbe demu wa sasa wa Cristiano Ronaldo, mrembo Georgina Rodriguez 23, alikuwa msichana wa kawaida sana kabla ya kukutana na supastaa huyo.

 

KUMBE demu wa sasa wa Cristiano Ronaldo, mrembo Georgina Rodriguez 23, alikuwa msichana wa kawaida sana kabla ya kukutana na supastaa huyo.

Taarifa zinaarifu kuwa Mhispania Georgina aliwahi kuwa ‘mboch’ yaani kijakazi au ukipenda yaya kule Bristol, Uingereza.

Kabla ya kuwa yaya, Uingereza, aliwahi kufanya kazi kwao Madrid kama mhudumu wa baa moja ya kifahari kwa jina Sansanet na pia muuza duka kwenye duka la fasheni la Gucci.

Mwaka mmoja kabla hajaanza kutoka kimapenzi na staa huyo tajiri wa kutupwa, Georgina alikuwa jijini Bristol akifanya kazi ya uyaya kwenye familia moja.

Baadaye familia hiyo aliyokuwa akiishi nayo Georgina ikawa inahamia nchi nyingine na hapo ikamlazimu kutengeneza bango la tangazo akiomba kazi ya aina yoyote ikiwamo hiyo ya uyaya aliyokuwa akifanya.

Bango hilo la tangazo akiomba kazi aliliposti kwenye gazeti la East Dulwich Forum Oktoba 2015 alikotoa maelezo akisema, “Kwa sasa naishi Bristol, Uingereza na familia moja ninayoilelea mabinti pacha. Nimekuwa na wakati mzuri kwa muda ambao nimekuwa nao. Sasa familia hii inahamia nchi nyingine na ninatafuta kazi katika familia nyingine nzuri ili niweze kutengeneza kumbukumbu tamutamu pia na wao. Kingereza changu ni cha wastani ila ninajitahidi sana kukielewa vyema. Mimi ni msichana ninayejiamni na siwezi kushindwa kutangamana na watu. Natumai nitapata fursa hii ninayoisaka. Kwa kungezea pia niko radhi kusaidia kwa kazi za ndani kando na uyaya tu.”

Kwa mujibu wa tangazo hilo, Georgina alikuwa akitazamia kupata kazi kufikia Januari 2016 kwakati familia aliyokuwa akiishia nayo ingekuwa ikihama.

Ni kipindi hiki ambapo ndipo alikutana na CR7 na kuanzisha uhusiano wa kisiri kwa miezi kadhaa kabla ya kuamua kuyaanika wazi.

Wawili hao walikutana kwenye pati moja ya fasheni ya Dolce & Gabbana ambapo CR7 alipagawishwa na urembo wake na kuamua kumtongoza.