http://www.swahilihub.com/image/view/-/4612680/medRes/2009183/-/mcwh50/-/pilamboga.jpg

 

Kuandaa pilau ya mboga

Pilau ya mboga.

Pilau ya mboga. Picha/MARGARET MAINA 

Na MARGARET MAINA

Imepakiwa - Thursday, June 14  2018 at  16:44

Kwa Muhtasari

Pilau ya mboga.

 

Kuandaa: Dakika 20

Mapishi: Dakika 40

Walaji: 4

 

Vinavyohitajika

 • Mchele wa kupikia biriyani.

 • Bizari nyembamba

 • Kitunguu

 • Nyanya 3

 • Tangawizi 1

 • Vitunguu saumu 2

 • Viungo vya pilau (chaguo lako)

 • Karafuu

 • Pilipili manga

 • Karoti

 • Majani ya ‘corriander’

 • Pilipili mboga

 • Kolimaua

Utaratibu

 • Menya vitunguu na uvikate upendavyo, kisha weka kwenye bakuli.

 • Osha nyanya na uvikate vipande vinne kwa kila nyanya

 • Osha na kisha kwangua kiasi cha karoti na nyingine kata vipande vidogo.

 • Osha kolimaua na itoe kwenye shina ili upate maua yake.

 • Menya tangawizi na kisha ikwangue

 • Menya vitunguu saumu kisha uvitwange.

 • Andaa viungo vyote vya pilau pembeni tayari kutumika

 • Osha na kisha andaa karafuu na pilipili manga

 • Bandika sufuria jikoni kisha uweke mafuta ya kupikia. Weka viungo vya pilau vya unga kisha weka bizari na kaanga kwa muda kiasi.

 • Weka kitunguu saumu , koroga kiasi. Weka tangawizi na endelea kukoroga. Weka kitunguu kisha koroga kwa muda kiasi. Acha viive kabla na kuanza kubadilika rangi.

 • Weka nyanya, chumvi, na pilipili manga. Koroga na kisha acha vichemke kwa dakika chache.

 • Weka karafuu, karoti, pilipili hoho na kolimaua Endelea kukaanga kwa  muda wa dakika kama 10.

 • Weka mchele huku ukiendelea kukaanga ili mchele wako uchanganyike vizuri na viungo kwenye sufuria.

 • Weka maji kulingana na kiasi cha mchele wako.

 • Weka moto wa wastani na kisha funika sufuria chakula kiive. Baada ya dakika 10 au 15 geuza pilau lako kisha weka majani ya ‘corriander’ ili kuongeza ladha na harufu nzuri ya chakula. Funika chakula ili kiendelee kuiva.

Subiri kwa muda wa dakika 10 na chakula kitakuwa tayari kuliwa.