http://www.swahilihub.com/image/view/-/4701572/medRes/2071858/-/o59yaj/-/zitui.jpg

 

Urembo wa nywele, kucha na ngozi

Nywele

Nywele za kupendeza ambazo hazijatiwa kemikali yoyote katika Queens Salon, Nairobi. Picha/MARTIN MUKANGU 

Na MARGARET MAINA

Imepakiwa - Tuesday, August 7  2018 at  12:17

Kwa Muhtasari

Mwonekano wa ngozi yako unatoa taswira kamili ya jinsi ulivyo kiafya ndani ya mwili wako.

 

MWONEKANO wa ngozi yako unatoa taswira kamili ya jinsi ulivyo kiafya ndani ya mwili wako.

Mara nyingi tumejitahidi sana ama kuondoa magonjwa au matatizo ya ngozi kwa kupaka dawa katika ngozi.

Mara nyingi huenda tukaonekana tumepona ila baada ya muda tena ile hali inajirudia.

Tunatafuta dawa nyingine tofauti lakini matokeo ni yaleyale.

Mwonekano usioridhisha wa ngozi yako ni matokeo ya mwili wako kuwa na taka sumu (toxins) ambazo huziba tishu za mwili wako na kusababisha mwili kuwa na madoa au ugonjwa wa ngozi. Pengine utajiuliza sasa nifanye nini ngozi yangu iwe na mwonekano mzuri wa kuvutia. 

Fanya yafuatayo:

1. Kula vyakula vinavyoleta na kuboresha afya ya ngozi. Vyakula hivi ni pamoja na dark orange beta carotene-rich foods kama vile karoti, maboga, viazi vitamu, karakara, parachichi, maharage na yoghurt na mboga za majani kama vile kabeji na spinachi. Kula samaki kama vile dagaa, salmon, tumia mafuta ya mizeituni katika saladi au kupikia.

2. Epuka au punguza ulaji wa vyakula vilivyokaangwa, vyakula vyenye wanga, vyakula vya ngano, nyanya, matunda aina ya machungwa, chokoleti, strawberries, karanga na bidhaa yake (peanut butter) na vyakula vyenye mafuta mengi.

3. Epuka kula kupita kiasi. Kula zaidi hufanya damu nyingi kusukumwa kwenda tumboni ili kusaidia uyeyushaji wa chakula hivyo ngozi kukosa mzunguko wa kutosha wa damu. Hali hii huikosesha ngozi viini lishe katika kiwango kinachotakiwa.

4. Kunywa juisi ya karoti, beet, celery, spinachi na tango ili kuleta mng'aro wa ngozi.

5. Usikose kunywa angalau glasi nane za maji kila siku. Unaweza kukamulia limau au ndimu katika maji kwani juisi yake itasaidia damu kutembea vizuri mwilini.

6. Kuwa makini na unywaji wa vinywaji vyenye kilevi, vinywaji baridi vyenye caffeine na kahawa kwa kuwa hupunguza kiasi cha maji katika mwili.


7. Vaa nguo zilizotengenezwa kwa nyuzi za asili kama vile pamba.

8. Kila siku jipumzishe angalau kwa dakika kumi. Hewa ya asili ni dawa ya ngozi ya bure.

9. Fanya mazoezi ya viungo. Husaidia kutoa uchafu mwilini kwa njia ya ngozi. Pia huzalisha joto ambalo huua bakteria wenye madhara waliopo katika ngozi.