MAPISHI: Mahamri

Mahamri

MAPISHI: Mahamri. Picha/MARGARET MAINA 

Imepakiwa - Friday, January 11  2019 at  10:59

Kwa Muhtasari

Andaa mahamri kwa kufuata utaratibu ufuatao.

 


MAPISHI: Mahamri

Muda wa kuandaa: Dakika 50

Muda wa mapishi: Dakika 30

Walaji: 5

Vinavyohitajika

Vikombe 3 vya unga wa ngano

Kikombe 1 maziwa ya ufufutende

½ kikombe sukari

½ kikombe maziwa ya unga

Mayai 2

Kijiko 1 cha  baking powder

½ kijiko cha hiliki ya unga

lita moja mafuta ya kupikia

½ kikombe maji

1 kijiko cha chai sukari


Namna ya k utayarisha Na Kupika 


Weka mchanganyiko wa hamira katika bakuli dogo kisha koroga na acha uumuke kiasi dakika 5. Ukitaka hamira iumuke haraka,

Washa microwave kiasi dakika 3 bila ya kitu ndani yake. Kisha weka mchanganyiko wa hamira ndani uache uumuke


Mchanganyiko wa mahamri

Changanya vitu vyote katika bakuli la kukandia unga kisha tia mchanganyiko wa hamira.

Washa mashine ikande unga kwa mpigo wa wastani kwa muda wa dakika nane mpaka donge la unga liwe laini.

Paka mafuta au unga mikononi kisha toa donge la unga ugawe madonge tisa.

Tandaza kila donge huku unanyunyizia unga ili usigande.

Lishepu vizuri tayari kwa maandalizi ya kusukuma na kukata.

Likishatandazika likawa duara ya kiasi lisiwe nene, kata donge sehemu 4 za shape ya pembe tatu.

Yaache kwa muda wa dakika 10 baada ya kuyakata yaumuke kisha itakua tayari kwa kuyachoma.

Pasha mafuta yako katika moto wa wastani yasiwe na moto mkali utafanya mahamri yako kuungua kisha yaweke katika moto na geuza kila mara ili yasivimbe upande mmoja na ikawa vigumu kuyageuza.

Yakiiva pande zote na kua na rangi ya kahawia,epuaa na uyaache yapoe kabla ya kupakua na ufurahie na kinywaji chochote ukipendacho.

Je, ungependa kujifunza kuandaa chakula kipi? Tuandikie kwa kutumia baruapepe: swahilihub@ke.nationmedia.com