http://www.swahilihub.com/image/view/-/4611576/medRes/2008344/-/qn0rghz/-/asali.jpg

 

Manufaa ya asali kwenye ngozi na nywele

Kenneth Agunga

Kenneth Agunga apakia asali kwa vipimo vya 250g, 500g, na kilo moja mjini ya kuuza Homa Bay, Mbita, Kisumu, Nakuru, na Nairobi. Picha/MAKTABA 

Na MARGARET MAINA

Imepakiwa - Thursday, June 14  2018 at  10:37

Kwa Muhtasari

Asali hutumika kulainisha ngozi kwa kuwa ina uwezo wa kuvuta unyevu kutoka kwenye hewa na kuipa ngozi uwezo wa kuhifadhi unyevu na hivyo ni muhimu kwa mtu mwenye ngozi kavu.

 


ASALI hutumika kulainisha ngozi kwa kuwa ina uwezo wa kuvuta unyevu kutoka kwenye hewa na kuipa ngozi uwezo wa kuhifadhi unyevu na hivyo ni muhimu kwa mtu mwenye ngozi kavu.


Jinsi ya kuandaa

Chukua asali halisi kijiko kimoja cha chai kisha paka usoni, kaa hivyo kwa dakika 15 hadi 20 kisha safisha uso wako.

Kulingana na Bi Jeniffer Nafula ambaye ameitumia asali kwenye uso wake kwa muda baada ya ngozi kuharibika alipotumia mafuta yenye kemikali, hajutii kutumia njia hii ya asili kwa uso wake.

“Nimeitumia asali usoni kwa miaka mitatu sasa. Najipaka angalau kila Jumamosi na baada ya kuiosha kutoka usoni mwangu, huwa napaka mafuta na uso na ngozi inakuwa nyororo,” anasema Bi Nafula.


Asali katika kusafisha ngozi, kutibu na kuzuia chunusi

Kutokana na uwezo wa asali wa kuua bakteria na kuvuta uchafu kutoka kwenye matundu ya ngozi, asali itakusaidia kutatua tatizo la chunusi.

Jinsi ya kuandaa

Chukua asali kijiko kimoja cha chakula; changanya na mafuta ya nazi au ya 'olive’ vijiko viwili.

Koroga hadi mchanganyiko uwe laini kisha paka usoni huku ukisugua taratibu kwa kufanya kama viduara huku ukiepuka kufikisha machoni.

Ukimaliza kusugua uso kwa mchanganyiko wako, osha uso wako.

Jinsi ya kuandaa kama kisafisha ngozi, ‘exfoliator'

Changanya kijiko kimoja asali na kijiko kimoja baking soda. tumia mchanganyiko huu kusugua ngozi yako. Asali inaongeza lishe inayozuia madhara yanayotokana na sumu za hewani zinazozeesha ngozi. Hamira au baking soda inasaidia kusafisha matundu ya ngozi. Pia inasaidia ngozi iliyoungua na jua kurudi katika hali nzuri ya kung'aa. 

 

Jinsi ya kutumia asali katika nywele

Asali inatibu nywele kavu na kulainisha ngozi kavu ya kichwa na kutibu muwasho kichwani.  


Jinsi ya kufanya

Changanya kijiko kikubwa cha asali na maji ya uvuguvugu kisha paka kichwani Acha kwa muda wa saa 1 iwe kama ‘conditioner’ kisha safisha nywele zako. Unaweza pia kuchanganya asali kiasi ya kijiko kimoja au viwili katika maji vikombe vitano kisha utumie kusafishia nywele zako taratibu, yaani yapitishe tu hayo maji kwenye nywele zako ambazo ni safi.

Tahadhari: Asali kwa kiasi kikubwa hupausha weusi wa nywele kutokana na Hydrogen Peroxide inayopatikana ndani ya asali. Ni vyema ukatumia asali mbichi kujihakikishia faida za asali katika mwili wako.