http://www.swahilihub.com/image/view/-/4791364/medRes/2130886/-/t3o9tm/-/karoti.jpg

 

Manufaa ya karoti katika urembo

Karoti

Karoti. Picha/MAKTABA 

Na MARGARET MAINA

Imepakiwa - Thursday, October 4  2018 at  13:45

Kwa Muhtasari

Maski ya uso kutumia karoti inafaa kwa aina yoyote ya ngozi kwa kuwa ina “antiseptic’ ya asili na haina kemikali yoyote inayoweza kudhuru ngozi yako.

 

WENGI wetu tunajua karoti kama tu ya kuliwa kwa namna mbalimbali kama vile, ikiwa mbichi kwa kutafuna, inaweza kupikwa na kuchanganywa na mboga zingine, inaweza kusagwa na kupata juisi ambayo pia inaweza kuchanganywa na juisi zingine, aidha kukatwakatwa na kuchanganywa kwenye salad ya matunda.

Lakini pia karoti inaweza kutumika katika urembo.

Maski ya uso kutumia karoti inafaa kwa aina yoyote ya ngozi kwa kuwa ina “antiseptic’ ya asili na haina kemikali yoyote inayoweza kudhuru ngozi yako.

Pia ina Vitamini C, E na Potassium ambayo husaidia kuipa ngozi unyevu.

Unahitaji

  • Karoti moja

  • Mtindi kijiko 1

  • Juisi ya limau vijiko 2

Cha kufanya

Kata karoti na uichemshe kwa dakika 10 kisha weka kwenye blenda utengeneze rojo.

Chukua rojo uipake usoni.

Kaa nayo kwa dakika 30.

Kamua uso wako kwa maji ya ufufutende kisha ufute kwa taulo safi kabla ya kupaka mafuta.

Tumia juisi ya karoti kuondoa mikunjo usoni.Karoti ina virutubisho muhimu kwa ngozi .

Chukua karoti, saga kwenye blenda kisha kamua ili upate juisi yake.

Tumia pamba kupaka juisi kwenye sehemu iliyo na makunyanzi.fanya hivi angalau mara mbili kwa wiki utaona mabadiliko.

Karoti ina Vitamini A inayosaidia ngozi isipate makovu meusi yatokanayo na chunusi na pia huzuia kuunguzwa na miale ya jua.