http://www.swahilihub.com/image/view/-/4706680/medRes/2075237/-/u0jaxnz/-/korogo.jpg

 

Maski ya parachichi na yai ni muhimu na huifanya ngozi iwe nyeupe na nyororo

parachichi na yai

Mwanadada akiwa amejipaka 'maski' ya parachichi na yai lililokorogwa. Picha/MAKTABA 

Na MARGARET MAINA

Imepakiwa - Friday, August 10  2018 at  11:50

Kwa Muhtasari

Watu wengi wana mazoea ya kutumia mkorogo wa parachichi na yai ambao wanapaka mwilini ili kuifanya ngozi iwe nyeupe na nyororo.

 

MCHANGANYIKO wa parachichi na yai lililokorogwa huwa ni mzuri kwa ngozi ya mafuta mengi na pia yenye chunusi.

Parachichi huipa ngozi unyevu huku yai likisaidia kuimarisha ngozi, kudhibiti mafuta kwenye ngozi na kupunguza makunyanzi.

Parachichi na yai ni mzuri kwa ngozi yako kwa sababu parachichi husheheni vitamini na madini. Huwa na vitamini E, mafuta yenye afya na ya asili.

Mkorogo huu huhifadhi unyevu katika seli za ngozi; huzuia kuzeeka mapema kwa kupigana na kiradikali bure ambayo husababisha makunyanzi na mistari ngozini kwa kuiba oksijeni kutoka seli za ngozi nzuri; na pia huwa na uwezo wa kupambana na ile hali ya ngozi kuungua ovyoovyo.

Yai huwa na protini, multivitamin na madini na ni muhimu katika kusafisha ngozi. Yai huwa na lysozyme ambayo hupambana na chunusi zinazosababishwa na bakteria. Huimarisha ngozi na hupunguza mashimo makubwa ngozini. Pia hupigana na kiradikali bure ambazo husababisha ile hali ya 'kuzeeka' au kuonekana kuzeeka mapema.

 

Jinsi ya kutengeneza maski ya parachichi na yai

Vitu unavyohitaji:

  • Parachichi lilopondwa kijiko kimoja

  • Yai

  • Bakuli la kuchanganyia

  • Uma

Andaa vitu vyote unavyovihitaji; yaani bakuli, yai, parachichi na uma kwa ajili ya kuchanganyia.

Ndani ya bakuli dogo pondaponda parachichi lako kisha ongezea yai halafu changanya vizuri kwa kutumia uma.

Changanya kila kitu kwa sekunde 30.

 

Jinsi ya kupaka

Osha uso wako vizuri na kuondoa vipodozi vinginevyo na uchafu wowote usoni. Tumia maji moto kiasi kusaidia kufungua mashimo (pores). Pangusa uso wako kwa kitambaa safi.

Tumia vidole vyako kuchukua mchanganyiko wako na kupaka usoni taratibu. Epuka sehemu za macho na midomo.

Iache maski yako usoni kwa dakika 10 hadi 15 hivi.

Muda huu ukishakamilika, osha uso kwa maji baridi, moisturise uso wako kwa kutumia mafuta ya mizeituni au mafuta ya nazi.