Tutumie vizuri michuano ya Kombe la Chalenji

Na TAHARIRI YA MWANANCHI

Imepakiwa - Tuesday, November 14  2017 at  15:34

Kwa Muhtasari

Michuano ya Kombe la Chalenji inatarajiwa kuanza Novemba 24 hadi Desemba 6 nchini Kenya.

 

MICHUANO ya Kombe la Chalenji inatarajiwa kuanza Novemba 24 hadi Desemba 6 nchini Kenya.

Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) ndiyo waendeshaji wa michuano hiyo inayfanyika kila mwaka katika nchi tofauti anapopatikana mdhamini.

Michuano hiyo itafanyika baada ya kupita miaka miwili bila kuchezwa na Tanzania imethibitisha kupeleka timu za wanaume na wanawake.

Pia, Tanzania imethibitisha kushiriki Kombe la Chalenji kwa timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 itakaoyofanyika Bujumbura, Burundi kuanzia Desemba 12 hadi 22.

Mbali na Tanzania Bara, pia zimo Zanzibar, Uganda, Kenya, Burundi, Rwanda Sudan Kusini, Ethiopia, Zimabwe na Libya ni waalikwa.

Tanzania Bara inawakilishwa na Timu ya Kilimanjaro Stars na Zanzibar ni Zanzibar Heroes.

Mara ya mwisho Tanzania Stars ilitwaa Kombe la Chalenji mwaka 2000 baada ya kuifunga Ivory Coast bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa makubaliano ya timu zote zitakazoshriki Kombe la Chalenji zinatakiwa kupeleka kikosi kwanza lengo likiwa ni kuhakikisha kunakuwepo na ushindani na kukuza kiwango cha soka kwa Afrika Mashariki na Kati.

Tarehe rasmi ya kuanza michuano iyo imetangazwa na hivyo ni jukumu la Tanzania kujiandaa vyema kushindnna na hatimaye kutwaa ubingwa.

Timu za Taifa zinatakiwa kuanza maandalizi mapema ili kuwajengea wachezaji uwezo wa kufanya vyema katika mechi zao.

Hakuna njia ya mkato kwa timu kupata mafanikio kama haitafanya maandalizi ya kutsha kuwajenea  uwezo wa kucheza mechi zao kikamilifu n ikiwezekana kuleta kombe Tanzania.

Watanzania wana kiu ya ubingwa kwa kuwa hawajawahi kuzipokea timu kwa shangwe.

Ni muhimu kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuhakikisha linapata wachzaji wenye umri sahihi na  baadaye walisaidie Taifa wakati watakapofikia kiwang hicho. Suala hilo  ni muhimu kwa timu ya wanawake itakayoshiriki mashindano hayo. Ligi ya wanawake ni kubwa ambayo haiwezi kutoa picha halisi ya kiwango chetu cha soka.

Ni kweli kwamba tumechelewalakini challenji inafaa kutuamsha kuwa tunatakiwa tuwe na mashindano sahihi yatakayotuwezesha kupata timu nzuri ya Taifa.

TFF inatakiwa iwe na mkakati wa jinsi ya kuyatumia mashindano ya Cecaf ambayo yamefufuliwa. Je ni mashindano ni mashndano ambayo yametullazimisha kuwaita kina Mbwana samatta na wengine walioko barani Ulaya au kuwajaribu wachzajiwa ndani?

Ni muhimu TFF ikawa na sera amay  itamsaidia koha kuandaa timu kulinana na malengo ya Shirikisho. Ili tmu ya Taifa iwe nnzuri kocha anatakiwa awajaribu wachezaji wengi kadiri awezavy na atafanikisha hilo kama atakuwa na mashndano mengi.