http://www.swahilihub.com/image/view/-/4843924/medRes/2165118/-/dgj930z/-/yoga.jpg

 

Njia kadha za kuondoa sumu ‘toxins’ mwilini

Mazoezi

Mtu akifanya mazoezi ya yoga. Picha/HISANI 

Na MARGARET MAINA

Imepakiwa - Friday, November 9  2018 at  11:37

Kwa Muhtasari

Mwili unapokuwa na sumu, hali ya kiafya inadorora pakubwa.

 

MARADHI mengi yanayowasumbua watu yanatokana na sumu zilizopo katika miili.

Sumu hizi hutokana na vyakula, vinywaji na hata mazingira tunamoyoishi.

Inatujuzu kufanya mambo kadha angalau kuondoa au kupunguza sumu katika miili yetu.

Kula vyakula vya asili

Ili kuweza kuondoa sumu mwilini mwako ni vyema ukaepuka vyakula ambavyo vina viini vinavyojenga sumu mwilini.  kula vyakula vya asili. Kama matunda na mboga.

Kunywa maji

Miili yetu imejengwa kwa maji asilimia 70, hivyo kunywa vinywaji kama vile soda na juisi kwa kiasi fulani huongeza sumu mwilini.

Ufanyaji kazi wa viungo kama vile figo hutegemea uwepo wa maji ya kutosha mwilini.

Fanya mazoezi

Watu wengi hawapendi kufanya mazoezi. Kufanya mazoezi kutawezesha viungo vyako vya mwili kufanya kazi ipasavyo. Unapofanya mazoezi utatokwa na jasho. hii ni njia nzuri ya kutoa sumu mwilini.

Punguza mafuta

Jizoeshe kupunguza ama kuepuka mafuta katika vyakula unavyokula kwani si aina zote za mafuta zinafaa kwenye mwili wako.

Kula vyakula vya ‘fibre’

Fahamu kuwa vyakula vyenye nyuzinyuzi ni vizuri pia katika kusafisha mwili na kuondoa sumu. Vyakula vyenye nyuzinyuzi ni kama parachichi, ndizi, karoti, pilipili mboga na kunde. Ulaji wa vyakula hivi utakuwezesha kuondoa kiasi kikubwa cha sumu mwilini.

Tambua na kuelewa vyema bidhaa unazozitumia

Elewa kila chakula au kinywaji unachotumia kina nini ndani yake. Vinywaji vingine na vyakula vina viambata ambavyo ni sumu katika mwili wako.