http://www.swahilihub.com/image/view/-/4610026/medRes/2007694/-/129u692/-/kimakula.jpg

 

Mapishi: Kuandaa nyama iliyosagwa

Kima

Kima ndiyo kitomeo cha nyama iliyosagwa. Picha/HISANI 

Na MARGARET MAINA

Imepakiwa - Wednesday, June 13  2018 at  12:38

Kwa Muhtasari

Kima ndiyo kitomeo cha nyama iliyosagwa.

 

Kuandaa: Dakika 12

Mapishi: Dakika 30

Walaji: 4

 

KUNA njia tofauti za kuandaa nyama ya kusaga. Kuna baadhi wanaoiosha na kuchuja maji na wengine wanachemsha.

Mimi huiandaa tofauti.


Vinavyohitajika

 • Nyama ya kusaga kilo 1
 • Vitunguu 2 vya kawaida
 • Vitunguu saumu 2
 • Tangawizi 1
 • Nyanya 4
 • Mafuta ¼ lita
 • Chumvi kijiko 1 cha chai
 • Karoti 2
 • Pilipili mboga 1
 • Ndimu 1

Maelekezo

 •  Menya vitunguu kuondoa matawi hafifu na ukate viwe kwenye vipande vyembamba sana
 • Menya karoti iwe kama uji
 • Menya pilipili mboga na kisha kata vipande vyembamba
 • Menya nyanya na zikate kawaida
 • Menya, osha na kisha kwangua tangawizi
 • Twanga vitunguu saumu
 • Bandika sufuria ya kupikia jikoni
 • Weka nyama na anza kukoroga ili kuzuia isigandie kwenye sufuria na kuungua
 • Weka kitunguu huku ukiendelea kukoroga kwa muda wa dakika 10
 • Weka kitunguu saumu na tangawiizi. Endela kukoroga kwa muda wa dakika 5 zaidi.
 • Weka mafuta kidogo sana ili kufanya viungo viize.
 • Weka pilipili mboga, karoti na kamulia ndimu. Ongeza chumvi kidogo. Endelea kukoroga.
 • Weka nyanya, koroga na funika sufuria kwa muda kama dakika 10.
 • Funua angalia kama imeiva.

 

Unaweza ipakua na wali, matoke, chapati au chochoke ukipendacho.