http://www.swahilihub.com/image/view/-/3815106/medRes/1565349/-/wklgq/-/huya.jpg

 

Mswazzi Masauti: Papa wa bahari ya muziki

Mswazzi Masauti

Ali Mohamed Said al-maarufu Mswazzi Masauti ni mwanamuziki maarufu nchini Kenya. Picha/PAULINE ONGAJI 

Na PAULINE ONGAJI

Imepakiwa - Thursday, February 16  2017 at  11:36

Kwa Mukhtasari

Alipobisha rasmi katika ukumbi wa muziki nchini, wengi walimwona Mswazzi Masauti kama samaki mdogo kutoka Pwani anayejaribu kuogelea.

 

ALIPOBISHA rasmi katika ukumbi wa muziki nchini, wengi walimwona kama samaki mdogo kutoka Pwani anayejaribu kuogelea.

Katika kipindi cha miaka kadha sasa Ali Mohamed Said al-maarufu Mswazzi Masauti amedhihirisha kuwa yeye ni papa katika tasnia hii ya muziki huku nyimbo zake zikiendelea kuvutia mashabiki sio tu hapa nchini bali Afrika Mashariki yote.

Kinamchomtenga na wasanii wengine ni ujuzi wake wa kugusia masuala ya kawaida maishani kupitia utunzi, ustadi ambao unazidi kukolea katika utunzi wake licha ya umri wake mdogo wa miaka 22 pekee.

Ujumbe unaotawala nyimbo zake unaambatana na yale anayotazama na kushuhudia kupitia kwa marafiki, jamaa na majirani huku vibao vyake kwa kawaida vikizungumzia masuala ya mapenzi.

Hasa anafahamika kwa vibao kama vile Mahabuba, wimbo wimbo ambao ulimvunia mashabiki nchini na mbali na hata kuwafanya wengi kumpigia upatu kushindania usawa ushabiki wa muziki wa bongo hapa nchini.

Wimbo huu ulimfikisha katika kiwango kingine kama mwanamuziki kwani wengi wanahoji kuwa ndio uliomtambulisha kwa mashabiki hasa ikizingatiwa kuwa ulichezwa pia nchini Tanzania.

Kadhalika anatambulika kwa nyimbo kama vile Siwezi na Usikate Tamaa, nyimbo ambazo kadhalika zinapitisha ujumbe wa maisha halisi ya kila siku.

Alianza kuimba mwaka wa 2007 na kufanya kibao chake cha kwanza mwaka huo lakini hakikutolewa.

Hata hivyo alianza kufanya vyema kati ya mwaka wa 2014 na 2015 baada ya kukutana na produsa Ian Michapo wa Mombasa ambapo alimrekodia vibao, Siwezi, mwaka wa 2014 na Usikate Tamaa, mwaka wa 2015.

Urafiki

Baadaye rafiki yake alimtambulisha kwa produsa J Blessings aliyefurahishwa na kazi yake na kumrekodia video za vibao hivi viwili.

Haikuwa muda kabla ya msanii huyu kunasa jicho la produsa matata, Tedd Josiah, aliyemsajili katika lebo ya SwaRnB, aliyefurahishwa na kibao chake kilichokuwa kimechapishwa mtandaoni.

Mzaliwa wa eneo la kisauni mjini Mombasa, Mswazzi alilazimika kuacha shule akiwa kidato cha pili kutokana na ukosefu wa karo.

Ni suala lililomlazimisha kufanya kazi mbali mbali za sulubu lakini hilo halikuzima ndoto yake ya kuwa msanii.