http://www.swahilihub.com/image/view/-/4878706/medRes/2187104/-/dcokh9/-/kwinikeki.jpg

 

MAPISHI: Queencakes za ndizi mbivu

Queencakes za ndizi mbivu.

Queencakes za ndizi mbivu. Picha/MARGARET MAINA 

Na MARGARET MAINA

Imepakiwa - Monday, December 3  2018 at  10:01

Kwa Muhtasari

Queencakes za ndizi zina ladha ya kipekee.

 

MAPISHI: Queencakes za ndizi mbivu


Muda wa kuandaa: Dakika 30

Muda wa kupika: Dakika 30

Walaji: 5


Vinavyohitajika

  • unga wa ngano gramu 400
  • sukari
  • kijiko 1 cha baking powder
  • kijiko ½  cha baking soda
  • kijiko ¼ cha chumvi
  • mafuta ya kupikia
  • ndizi 6 mbivu (zigandishe kwenye jokovu)
  • kijiko ½ cha vanilla essence
  • korosho au karanga za kuoka

Maelekezo

Washa ovena yako katika moto wa nyuzi 350.

Chukua chombo cha kuokea chenye mashimo 12 ya queencake kisha weka zile karatasi maalumu za kuokea.

Chukua bakuli safi na kavu kisha kwalo uchanganye unga wa ngano, sukari, baking powder na chumvi.

Zitoe ndizi ulizoweka kwenye jokovu kisha ziweke kando kwa dakika 20 ili zitoe barafu; au kwa lugha rahisi; barafu iyeyuke.

Menya ndizi na ziweke kwenye blenda uzisage mpaka upate rojo.

Sasa mwagia mchanganyiko wako wa ndizi kwenye mchanganyiko wa unga pamoja na mafuta ya karanga na vanilla. Tumia mwiko kuchanganya taratibu na polepole mpaka mchanganyiko wako ushikane vizuri.

Chukua kijiko kikubwa au mwiko kisha anza kumimina mchanganyiko wako kwenye mashimo ya queencake.

Oka kwa muda wa nusu saa.

Zitoe queencakes zako zikiwa bado katika zile karatasi maalumu za kuokea na ziweke kando zipoe.

Pakua na ufurahie.