Tunalo la kujifunza katika uchaguzi wa Kenya

Uhuru Kenyatta

Mgombea urais wa Jubilee Party, Uhuru Kenyatta, apiga kura Agosti 8, 2017 katika kituo cha Shule ya Msingi ya Mutomo, Gatundu, Kaunti ya Kiambu. Picha/PSCU 

Na MHARIRI – MWANANCHI

Imepakiwa - Thursday, August 10  2017 at  14:01

Kwa Mukhtasari

Juzi Wakenya walifanya Uchaguzi Mkuu wenye ushindani mkali kati ya chama tawala cha Jubilee na Muungano wa Vyama vya Upinzani vya Nasa.

 

JUZI Wakenya walifanya Uchaguzi Mkuu wenye ushindani mkali kati ya chama tawala cha Jubilee na Muungano wa Vyama vya Upinzani vya Nasa.

Si vibaya tukayatazama baadhi ya mambo yaliyotokea katika mchakato wa uchaguzi huu hasa yale ambayo tunaona yana tija katika uchaguzi ambayo ni mazuri kuyafanyia kazi katika kupanua wigo wa demokrasia yetu.

Pamoja na kwamba kila nchi ina uhuru wake na taratibu zake za kujiamulia mambo yake kwa mujibu wa sheria na Katiba yake, sisi tunadhani wakati mwingine inapobidi hakuna ubaya wowote kujifunza kutoka kwa wenzetu mambo ambayo ni mazuri kufanyia kazi kwa lengo la kujenga au kuboresha msingi uliopo.

Moja ya mambo hayo ni hatua ya raia wa Kenya walioko nje ya nchi hiyo kuruhusiwa kupiga kura za urais, jambo ambalo hapa kwetu halijawahi kufanyika na tunadhani kwamba si vibaya tukianza kuweka kwenye taratibu zetu kwa kuwa hatuoni sababu za misngi za kuwazuia.

Kwa bahati nzuri mfano huo unaonyeshwa katika ardhi yetu baada ya Wakenya walioko Tanzania kukusanyika katika Ubalozi wa Kenya jijini Dar es Salaam na wengine mkoani Arusha kushiriki kuchagua rais wao kama ilivyofanyika pia katika Uchaguzi Mkuu wa Rwanda uliomalizika wiki iliyopita.

Vyombo vyetu vya kutoa uamuzi na Tume ya Taifa ya Uchaguzi hapa nchini vikaanza kutafakari.

Jambo la pili ambalo limetokea nchini Kenya ambalo pia tunaamini linafaa kuigwa ni la wafungwa kushiriki uchaguzi wa urais wa nchi hiyo. Kwa muda mrefu hapa nchini hilo la wafungwa kupiga kura limekuwa limezungumzwa na wanaharakati lakini taratibu za kikatiba na kisheria hazijaliwezesha na sisi tunadhani kama ni baya kwa kuwa hata wafungwa ni raia wa nchi na wengi wao ama wataarithirika au kufaidika na uamuzi wa kiongozi anayechaguliwa.

Pamoja na hayo, ukiacha vurugu mbalimbali ziizojitokeza katika maneno machache kama Mombasa ambazo zinapaswa kulaaniwa na kupingwa. Pia utaratibu ulioanza kutangaza matokeo ya kura za urais haraka mara baada ya kuanza kuhesabiwa, nalo linawea kufanyiwa kazi na itaingizwa katika taratibu zetu.

Endapo suala la kuanza haraka kutangaza matokeo ya urais, litazingatiwa katika chaguzi zetu zijazo, bila shaka litasaidia kupungza taharuki ambayo isipodhitiwa itazaa fujo na hatimaye ghasia.

Ni imani yetu kwamba watendaji wa vyombo vyetu vya uchaguzi wameyaona masuala haya na kuyapima ili kuona uzuri na ubaya wake na hivyo kuchagua ni nini cha kuchukua na kipi cha kuacha ili tuwe n uchaguzi ulio bora zaidi.

Pamoja na kwamba si rahisi kumridhisha kila mtu katika uchaguzi, lakini mchakato unapofanyika kwa wazi na haraka, huweza kupunguza malalamiko ambayo hayana msingi.

Na hata pale malalamiko yanapotolewa unaona pia mahakama zinavyoyashughulikia kwa haraka na kuona mwongozo wa jinsi ya kuendana nayo na hatimaye kukamilishah azi kazi hiyo kwa amani.

Si vbaya kuyachukua mambo mazuri kutoka kwa wenzetu na ndio maana tunasisitiza kuwa kuna mambo mengine ya kujifunza kutoka Kenya katika uchaguzi wao ambao ulifanyika juzi.

Tahariri ya Mwananchi,

Mwananchi Communications Limited (MCL)

Tanzania.