http://www.swahilihub.com/image/view/-/4609586/medRes/2006823/-/14xmn5hz/-/oshaso.jpg

 

Urembo: Maski ya unga wa Chickenpea

Mwanamke wa Kiafrika aosha uso wake

Mwanamke wa Kiafrika aosha uso wake. Picha/MAKTABA 

Na MARGARET MAINA

Imepakiwa - Friday, October 5  2018 at  10:35

Kwa Muhtasari

Unaweza ukatumia unga wa Chickenpea kung'arisha uso wako.

 

Maski ya unga wa Chickenpea

VITU vingi jikoni mwetu vina manufaa katika urembo. Kupika bajia ukitumia unga wa chickenpea ni jambo la kawaida sana kwa wengi ila pia unaweza kuitumia katika ngozi na itakuwacha na mng’ao.

Vinavyohitajika

  • Vijiko 3 vya unga wa Chickenpea

  • Yai 1

  • Juisi ya limau vijiko 2

Weka unga wa Chickenpea katika bakuli.

Vunja yai na utoe kiini. Changanya kiini na unga hadi mchanganyiko ulainike kabisa.

Osha uso kwa maji ya ufufutende na uukaushe kwa taulo safi.

Paka mchanganyiko huo usoni na shingoni.

Kaa nao kwa dakika 20 kabla ya kuosha uso wako tena.

Fanya hivi angalau mara mbili kwa wiki na utaona mabadiliko.

Kulingana na Diana Wangeci, mkazi wa Nakuru, yeye hutumia unga huu kwenye uso wake kama maski kwa kuwa ngozi yake ni 'sensitive' sana.

Namna nyingine

Vinavyohitajika

  • Vijiko 4 unga wa Chickenpea

  • Maziwa vijiko 2

  • Juisi ya limau kijiko 1

Changanya unga, maziwa na juisi ya limau.

Paka mchanganyiko huo usoni mwako au popote unapotaka kung’arisha.

Ni muhimu uuache mchanganyiko huo hadi utakapokauka.

Osha kwa maji moto kabla ya kufuta na kupaka ‘moisturiser’

Viungo vya asili havina kemikali inayoweza kudhuru ngozi yako.