http://www.swahilihub.com/image/view/-/4926046/medRes/2218392/-/292owrz/-/ikoiki.jpg

 

MAPISHI: Viazi vitamu vya kuchemsha

Viazi vitamu

Viazi vitamu. Picha/SAMMY WAWERU 

Na SAMMY WAWERU

Imepakiwa - Tuesday, January 8  2019 at  13:05

Kwa Muhtasari

Viazi vitamu ni mojawapo ya viazi asili vinavyopendwa na raia wa ukanda wa Afrika Mashariki, hasa wakati wa staftahi.

 

VIAZI vitamu vmesheheni wanga, fiber inayokabiliana na shida za kusokotwa na tumbo, na madini ya Potassium.

Pia, viazi hivi vinaaminika kudhibiti magonjwa kama ya; Kisukari, Afkani, Pumu na Saratani. Vina sukari hai yake ya kukua nayo.

Viazi hivi vinaweza kuandaliwa kwa njia kadha wa kadha, kama kuvichemsha, kuvichoma na kuna wanaovikaanga pamoja na viazimbatata na boga.

Katika makala hii tunaandaa viazi vitamu vya kuchemsha, muda wake wa maandalizi ukiwa karibu dakika 60; yaani muda wa saa moja.

Vinavyohitajika

  • Viazi vitamu, kulingana na kiasi kitakachomtosha mlaji ama walaji
  • Maji

Matayarisho

Andaa kwa kuosha viazi vyema kwa sababu huwa na udongo ama mchanga, kama vilivyotoka shambani.

Vitie kwenye chungu ama sufuria, vile vikubwa vikate ili viweze kutoshea. Weka maji yatakayozidi kiwango ambacho viazi vimefikia, kisha uinjike sufuria mekoni.

Wakati vikiendelea kutokota, geuza vilivyojuu virudi chini na vilivyochini, viwe juu. Uwe makini dhidi ya kuvitoboa.

Kwa muda wa dakika 60 hivi, vitakuwa tayari. Viepue, kamua maji halafu usubiri vipoe. Vichambue kwa kutoa maganda ya juu, vikatekate viwe vipande vitakavyotosha kutiwa kinywani.

Viazi tayari kuliwa kwa chai ya mkandaa, ya maziwa, au maziwa.

Maelezo ya picha

Viazi asili vitamu vilivyochemshwa kabla ya kuchambuliwa maganda, na baada.

Je, ungependa kujifunza kuandaa chakula kipi? Tuandikie kwa kutumia baruapepe: swahilihub@ke.nationmedia.com