http://www.swahilihub.com/image/view/-/4757672/medRes/2108646/-/xqbm8d/-/matumbua.jpg

 

MAPISHI: Vitumbua

Vitumbua

Vitumbua. Picha/MARGARET MAINA 

Na MARGARET MAINA

Imepakiwa - Thursday, September 13  2018 at  13:41

Kwa Muhtasari

Vitumbua huwa vitamu sana.

 


MAPISHI: Vitumbua

Maandalizi: Dakika 15
Kupika: Dakika 30
Walaji: 4

Vinavyohitajika

  • Unga wa ngano vikombe viwili
    Sukari robo kikombe

  • Baking powder kwa kipimo cha vijiko vinne vya chai
    ½ kijiko cha chai chumvi

  • Vikombe 1⅔ maziwa

  • ¼ kikombe, siagi iliyoyeyushwa

  • Vijiko 2 vya chai vanilla

  • Yai 1

Maelekezo

Kwenye bakuli kubwa, chekecha unga wa ngano, sukari, baking powder na chumvi. Changanya vizuri.

Ongeza maziwa, siagi iliyoyeyushwa, vanilla na yai. Changanya vizuri; ukianzia kukoroga katikati viungo vya majimaji mpaka unga ulainike vizuri kabisa.

Funika mchanganyiko huo na acha kwa muda wa hadi saa moja au zaidi.

Kwenye kikaangio kisichoshika chini, katika moto wa wastani, paka kikaangio siagi kiasi.

Mwagia ¼ kikombe ya unga kwenye kikaangio. (Kama unga ni mzito sana, ongeza maziwa kiasi kulainisha). Pika mpaka upande wa chini uwe kahawia, itune kwa juu.

Geuza, pika mpaka pande zote ziwe za kahawia.

Rudia kwa unga uliobakia hadi umalize.

Pakua na unachopenda.