http://www.swahilihub.com/image/view/-/2600394/medRes/929317/-/gktlm7z/-/papa_fumbwa.jpg

 

Wananchi Geita waunge mkono utafiti wa kaya maskini

Papa Francis akutana na watoto

Papa Francis akikutana na watoto katika hafla moja jijini Manila Januari16, 2015. Papa aliwataka viongozi Ufilipino kumaliza kashfa ya pengo kubwa kati ya matajiri na maskini. Picha | AFP 

Na TAHARIRI YA MWANANCHI

Imepakiwa - Thursday, February 8  2018 at  08:48

Kwa Muhtasari

Gazeti la Mwananchi toleo la Jumatano lilikuwa na habari iliyohusu mpango wa Serikali wa kuzifanyia utafiti wa kipato na matumizi wa kaya maskini 608 za mkoani Geita ambao ni utekelezaji wa mwongozo wa mpango wa maendeleo ya Taifa unaojulikana kama Dira ya Taifa na Maendeleo 2015.

 

GAZETI la Mwananchi toleo la Jumatano lilikuwa na habari iliyohusu mpango wa Serikali wa kuzifanyia utafiti wa kipato na matumizi wa kaya maskini 608 za mkoani Geita ambao ni utekelezaji wa mwongozo wa mpango wa maendeleo ya Taifa unaojulikana kama Dira ya Taifa na Maendeleo 2015.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Robert Gabriel alinukuliwa na Mwananchi akisema Takwimu hizo zitasaidia Serikali na wadau wengine kutathmini hatua zilizofikiwa katika malengo ya Taifa na kimataifa.

Gabriel alisema utafiti huo unatarajia kukusanya taarifa zinazohusu wanakaya, uzazi, unyonyeshaji, elimu na afya, lakini pia watafiti wataangalia masuala ya uhamiaji, ulemavu, bima, ajira, biashara na mapato ya kaya, matumizi ya nishati, huduma za fedha na upatikanaji wa chakula, kilimo na mifugo.

Mbali na Gabriel, meneja takwimu mkoani Geita Khalid Msabaha aliwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa kuwa utafiti huo ni muhimu kwa mipango ya maendeleo. Azma ya Serikali ni kuwa nchi ya viwanda na kuona uchumi unatoka ulipo kwenda kuwa uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Tunafahamu katika utekelezaji wa dira hiyo, Serikali iliandaa mpango wa miaka mitano na kuweka vipaumbele vyake ambavyo ni miundombinu ya nishati, usafirishaji, Tehama, maji safi na maji taka na Umwagiliaji.

Vipaumbele vingine ni kilimo cha mazao ya chakula na biashara, ufugaji, uvuvi, misitu, viwanda na hasa vinavyotumia malighafi ya ndani kwa maana ya kuongeza thamani viwanda vikubwa vya mbolea na saruji, kieletroniki na maendeleo ya rasilimali watu hasa kuinua stadi za kazi mkazo ukiwekwa katika masomo ya sayansi, teknolojia na ubunifu.

Pia Serikali imeweka mkazo katika kuimarisha mafanikio yaliyopatikana kutokana na utafiti wa kipato na matumizi katika kaya 34 za mkoani Geita. Kwa maana nyingine utafiti huo ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa.

Kutokana na hoja hizo ni muhimu wa mkoa huo kuwa na ushirikiano utakaofanikisha lengo la Serikali kwani maendeleo yoyote hayawezi kufikiwa bila kuwapo kwa takwimu za walengwa katika maendeleo yao.

Ushirikiano wa wananchi katika utafiti huu ndio utakatoa mwelekeo sahihi wa kutimiza malengo makuu ya kuifanya Serikali ifanikiwe kuifikisha Tanzania kwenye hadhi ya nchi yenye kipato cha kati na kuondokana na umaskini uliokithiri ifikapo mwaka 2025.

Tunafahamu malengo ya Serikali katika mpango huu ni kuwaletea wananchi maisha bora, kudumisha uongozi na utawala bora wa sheria na kujenga uchumi imara wenye uwezo wa kukabiliana na ushindani.

Hata hivyo rai yetu kwa watendaji wa Serikali wazingatie weledi katika utekelezaji wa jukumu lao la kufanya utafiti.

Tunaamini hatutasikia kashfa ya kuwapo kwa takwimu za kupika. Wahusika watafika maeneo yote ya mijini na vijijini bila kujali changamoto za usafiri na fedha.

Kuendendelea kwa Taifa la Tanzania kunategemea usahihi wa takwimu za kiwango cha umaskini nchini kwa kuwa Serikali ipo katika mchakato wa utekelezaji wa mpango wa maendeleo  ni wazi hakutakuwa na visingizio vya kukwamisha utafiti huo.

Juhudi zinazofanywa na Rais Magufuli za kuifanya Tanzania ya viwanda ni lazima ziungwe mkono kwa upatikanaji wa takwimu sahihi na kwa haraka zinazohusu kiwango cha umaskini nchini.

Tahariri ya Mwananchi,

Mwananchi Communications Limited (MCL)

S.L.P. 19754 Dar es Salaam-Tanzania

SIMU +255222450875 au +255754780647