http://www.swahilihub.com/image/view/-/5118054/medRes/2345544/-/tx88p0/-/mvua+pic.jpg

Mvua, bomoabomoa zinavyotuaibisha

Na Mwandishi wetu

Imepakiwa - Thursday, May 16  2019 at  13:26

Huwa tunajaribu kujisitiri kwa wageni wanaofika nchini kadri tunavyoweza. Tunajaribu kuficha aibu mbalimbali zinazotukabili. Hata hivyo, tumeshindwa kuwaficha ndugu wawili tu; mvua na bomoa bomoa.

Hapo katika mvua simaanishi mafuriko. Hayo ni mambo mawili tofauti. Kuna mvua halafu kuna mafuriko. Haya mafuriko huwa yanaletwa na mvua ‘iliyopitiliza’. Wakati mwingine hata Wazungu pamoja na kuendelea kwao huwa wanateswa na mafuriko.

Sisi huwa tunateswa sio na mvua zilizopitiliza pekee bali hata mvua za kawaida. Mvua ya dakika 20 tu inaweza kuleta mafuriko Dar es Salaam. Kisa? mipangilio ovyo ya jiji letu. Hatuna miundombinu ya kupeleka maji bahari na kwingineko yanakotakiwa kwenda.

Tumefeli kama watu binafsi, lakini pia Serikali imefeli. Inapokuja mvua kubwa kama ya sasa hali inakuwa mbaya zaidi. Lakini hapo hapo tukumbuke kwamba hata hizi mvua za sasa haziwezi kuwekwa katika kundi la mvua zilizopitiliza. Mvua za sasa zingekuwa katika baadhi ya nchi ambazo zina mipango mizuri ya miji wala zisingeleta athari.

Matatizo yanayoletwa na mvua huwa nayapima na matatizo ya bomoa bomoa. Inakuaje tunabomoa kila wakati tunapotaka kufanya ujenzi? Kwa sababu watu wa zamani hawakufikiria mambo yanayoweza kuja sasa. Na hata sisi hatufikirii mambo yanayoweza kuja mbele.

Hapa wenzetu huwa wanatucheka kwamba tuna akili ndogo ya kufikiria baadaye. Wageni wakija na kukuta bomoa bomoa wanatucheka. Wanasikitika hatukuwa na akili ya kufikiria mbele. Kama unabisha basi subiri tu. Baada ya miaka michache ijayo utasikia kule Tegeta, Goba, Bunju na kwingineko nje ya jiji kuna majumba yanavunjwa kupisha ujenzi.

Sidhani kama tumefikiria kwamba kuna siku tutahitaji barabara pana au reli katika maeneo hayo. Tumeacha wananchi wajenge bila ya kujua mahitaji yetu ya baadaye. Kwa nini tusitenge sasa maeneo ya barabara pana au njia za reli? Tumesubiri wananchi wanajenga lakini ipo siku utasikia tunabomoa majumba yao.

Hatuna mipango ya muda mrefu na ndio maana mvua na bomoa bomoa huwa zinatuaibisha. Wenzetu huwa wanajua kutabiri kinachoweza kutokea. Wanaingiza akili zao katika mipango miji.