Mvutano kati ya Marekani na China nani anaumia na vikwazo?

Imepakiwa - Wednesday, May 15  2019 at  13:03

 

Mvutano wa kiuchumi kati ya Marekani na China unazidi kushika kasi huku kampuni za Kimarekani zikielezwa zitaathirika zaidi.

Rais Donald Trump amesema mara kwa mara kwamba China italipa ushuru ulioongezwa, ingawa mshauri wake kiuchumi, Larry Kudlow anasema kampuni za Kimarekani ndizo zitalazimika kuzama zaidi mifukoni kugharimia ongezeko la ushuru.

Ijumaa iliyopita Marekani ilipandisha ushuru wa bidhaa za dola 250 bilioni zinazoingizwa China kutoka asilimia 10 hadi asilimia 25; China nayo ikatangaza ongezeko kwa bidhaa za Marekani kutoka asilimia tano hadi 25.

Mwanasheria katika kampuni ya Cooley LLP, Christophe Bond ameieleza BBC kuwa zitakaoumia ni kampuni za Marekani zinazoagiza bidhaakutoka  China zitakazolipa ushuru huo kama kodi kwa nchi yao.

Cooley ambaye alikuwa mwanasheria mwandamizi wa Serikali ya Canada wakati wa majadiliano ya ukanda uhuru wa kibiashara kati ya nchi hiyo na Umoja wa Ulaya (EU), amesema kuna uwezekano mzigo huo ukatupwa kwa watumiaji wa bidhaa nchini Marekani kupitia na ongezeko la bei.

“Ushuru huu una athari kubwa katika mnyororo mzima wa usambazaji bidhaa,” amsema. Kiwango cha bidhaa hizo kimepungua kwa asilimia 9 katika robo ya kwanza ya 2019, ikimaanisha mgogoro umeanza kung’ata.

Mtaalamu wa biashara kutoka Chuo kikuu cha Cambridge, amesema hakuna ushahidi kuwa kampuni za China zimepunguza bei ili kuwavutia wanunuzi wa Kimarekani, lakini wasafirishaji wa bidhaa muhimu wamepungua baada ya kampuni za Marekani kuagiza bidhaa mahali pengine.