Nigeria yakumbwa na majonzi

Waokoaji wakiendelea na shughuli ya uokoaji mjini Lagos Nigeria 

Imepakiwa - Friday, March 15  2019 at  13:55

 

Lagos. Wafanyakazi wa huduma za dharura mjini Lagos wanaendelea na kazi ya kuokoa maisha ya watu kutoka kwenye kifusi cha jengo lililoanguka Jumatano katika eneo la Ita-Faaji, Mji wa kibiashara.

Polisi iliithibitishia BBC kuwa mpaka sasa watu 50 wameokolewa huku wengine takribani 11 wakipoteza maisha.

Serikali jijini Lagos imesema uchunguzi utafanyika baada ya operesheni ya ukoaji kukamilika na kuhitimisha kuwa wale wote waliohusika watashtakiwa.