Red Cross yatoa onyo matumizi ya nembo yake

Na HAJI MTUMWA, Mwananchi

Imepakiwa - Friday, November 9  2018 at  13:52

Kwa Muhtasari

Wanaotumia nembo ya Red Cross kinyume na sharia kuuona moto wa jiwe visiwani Zanzibar.

 

VISIWANI ZANZIBAR

CHAMA cha Msalaba Mwekundu (Red Cross) Tanzania kimetoa onyo la kuwachukulia hatua za kisheria watu watakaotumia nembo ya chama hicho kinyume na sheria.

Rais wa chama hicho, Mwadini Abass Jecha alitoa onyo hilo wakati akizindua utoaji elimu ya matumizi bora ya nembo hiyo mjini Unguja juzi.

Alisema baadhi ya watu wamekuwa wakitumia nembo hiyo vibaya ikiwamo kuweka mbele ya magari na kwenye maeneo ambayo haipaswi kuwapo jambo ambalo ni kosa kwa mujibu wa sheria.

Kwa upande wake mratibu wa Red Cross, Ubwa Suleiman alisema chama hicho kinafanya kazi wakati wote kusaidia jamii.