http://www.swahilihub.com/image/view/-/4744612/medRes/2100157/-/gwycb9/-/kilela.jpg

 

Shein aeleza azma ya Serikali Zanzibar

Dkt Ali Mohamed Shein

Rais wa Zanzibar, Dkt Ali Mohamed Shein. Picha/MAKTABA 

Na HAJI MTUMWA

Imepakiwa - Thursday, January 31  2019 at  13:43

Kwa Muhtasari

Serikali Zanzibar inapanga kuanzisha taasisi ya utafiti ya uvuvi na mazao ya bahari ili kwenda sambamba na sera ya uchumi wa bahari.

 

UNGUJA

RAIS wa Zanzibar, Dkt Ali Mohamed Shein ameeleza azma ya Serikali yake kuanzisha taasisi ya utafiti ya uvuvi na mazao ya bahari ili kwenda sambamba na sera ya uchumi wa bahari.

Dkt Shein amesema kuna umuhimu mkubwa kwa Zanzibar kuwa na taasisi hiyo hasa ikizingatiwa mazingira na uchumi wake.

Amesema hayo wakati alipokutana na uongozi wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Ikulu mjini Unguja jana Jumatano.