TFDA wawanoa wafanyabiashara 100

Na SADA AMIR

Imepakiwa - Wednesday, June 13  2018 at  14:37

Kwa Muhtasari

Wajasiriamali 100 mkoani Mwanza wamefundishwa namna ya kubuni na kutengeneza vifungashio ili kuongeza thamani ya bidhaa zao.

 

MWANZA, Tanzania

ZAIDI ya wajasiriamali 100 kutoka halmashauri nane mkoani Mwanza, wamenolewa kuhusu udhibiti wa ubora wa bidhaa zao ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi.

Licha ya ubora wa bidhaa, wajasiriamali hao walifundishwa namna ya kubuni na kutengeneza vifungashio ili kuongeza thamani ya bidhaa zao.

Mafunzo hayo yalitolewa jijini Mwanza juzi na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo nchini (Sido).

Kaimu mkurugenzi wa udhibiti ubora wa TBS, Nikonia Mwambene alisema baada ya mafunzo hayo, bidhaa za wajasiriamali hao zitakaguliwa, kupimwa na kupewa leseni na nembo kuthibitisha ubora wake.

“Tunalenga kuziwezesha bidhaa za wajasiriamali nchini kupenya na kushindana ndani na nje ya soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC),” alisema Mwambene.