http://www.swahilihub.com/image/view/-/3734170/medRes/1540248/-/98xqs7z/-/unia.jpg

 

Ulaya tunasikia kwenye bomba – Ummy Mwalimu

Bi Ummy Mwalimu

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi Ummy Mwalimu akihutubia wanahabari Dar es Salaam, Januari 18, 2017. Picha/SWAHILI HUB 

Na MWANDISHI WETU

Imepakiwa - Monday, April 16  2018 at  13:24

Kwa Muhtasari

Waziri Ummy Mwalimu amesema katika Serikali ya Awamu ya Tano, mawaziri wanasikia Ulaya kwenye bomba; tofauti na zamani kwani kazi yao kwa sasa ni kutembelea wilaya kutatua kero za wananchi.

 

NZEGA, Tanzania

Waziri wa Afya, Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wazee  na Watoto Ummy Mwalimu amesema katika Serikali ya Awamu ya Tano, mawaziri wanasikia Ulaya kwenye bomba; tofauti na zamani kwani kazi yao kwa sasa ni kutembelea wilaya kutatua kero za wananchi.

Mwalimu aliyasema haya wakati akizindua kitu cha Afya cha Zogolo wilayani Nzega Mkoani Tabora ambacho kimeboreshwa kutokana na michango ya wizara yake ambayo imechangia Tsh500 bilioni, nguvu za wananchi na Mbunge wa Nzega mjini (CM) Bw Hussein Bashe.

“Zamani mlikuwa mmezoea mkitusikia kunakwenda Ulaya, China au kwingineko. Siku hizi tunakusikia tu kwenye bomba. Ndiyo maana leo niko hapa kusikiliza na kufungua kituo hiki,” alisema Waziri Ummy.

Pia aliwahamasisha kujiunga na bima mbalimbali za afya ili wapatiwe matibabu pale wanapougua.

Alisema kwa sasa bima hizo zinapatikana kwa kuazia Sh10,000 hivyo kila mwanachi akijali afya yake ataweza kuhudumiwa.

Akizungumza katika uzinduzi huo Bashe alisema kuwapo kwa kituo hicho cha afya na kufikia hadhi hiyo na kupatiwa gari la wagonjwa, umetokana na ahadi za Serikali ya Awamu ya Tano walipoomba kura mwaka 2015.

Alisema jambo hilo limeshatimia kwa asilimia 100 ikiwa sasa hivi wanasubiri maji yanayotoka Ziwa Victoria ili kutimiza ahadi nyingine muhimu.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alisema mkoa huo una upungugu wa wataalamu wa afya wakiwamo madaktari kwa asilimia 50.

Kutokana na hali hiyo, aliomba Serikali kuwasaidia kupata wataalamu hao ili wananchi waweze kupata huduma.