http://www.swahilihub.com/image/view/-/4611540/medRes/2008234/-/114v573/-/umila.jpg

Waziri agoma kuunda kamati kuchunguza MV Mapinduzi

Sira Ubwa Mamboya

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Bi Sira Ubwa Mamboya. Picha/HISANI 

Na HAJI MTUMWA, Mwananchi          hmtumwa@mwananchi.co.tz

Imepakiwa - Thursday, June 14  2018 at  10:29

Kwa Muhtasari

Mwakilishi wa Paje ataka kujua faida ya meli hiyo tangu iliponunuliwa na kuanza kazi

VISIWANI ZANZIBAR

WAZIRI wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, Sira Ubwa Mamboya, amesema hayupo tayari kuunda kamati maalumu kuchunguza Meli ya Mapinduzi (II) ambayo ipo kwenye matengenezo.

Sira alitoa kauli hiyo jana katika mkutano wa Baraza la Wawakilishi wakati akijibu swali la mwakilishi wa Paje, Jaku Hashim Ayoub aliyetaka kujua sababu za meli hiyo kuharibika kila mara na kutumia fedha nyingi kwa ajili ya matengenezo yake, huku akihoji kama waziri yupo tayari kuunda kamati maalumu kuichunguza na kujua undani wake.

Waziri Sira alisema suala la kuundwa kwa kamati maalumu ya kuchunguza meli hiyo halina nafasi kwa sasa kwa kuwa meli hiyo inaendelea na matengenezo.

Alisema kama wajumbe wa baraza hilo wanataka kuitembelea na kuikagua meli hiyo, wanapaswa wasubiri hadi itakapokamilika.

“Nipo tayari kuungana na wajumbe hata baraza zima kuikagua meli hiyo mara tu matengenezo yatakapokamilika, ila si kwa wakati huu ambao mafundi wanaendelea na matengenezo,” alisema Sira.

Faida ya meli

Pia, waziri huyo alijibu swali la msingi la Ayoub aliyetaka kujua faida ya meli hiyo tangu iliponunuliwa na kuanza kazi visiwani humo.

Alisema kuna faida lukuki zinazotokana na kuwapo kwa meli hiyo kwani kumekuwa na upatikanaji wa uhakika wa usafiri kati ya Unguja na Pemba.

Sira alisema katika kipindi cha Januari 2016 hadi Januari mwaka huu abiria 385,909 wamepata huduma ya usafiri wa meli hiyo.

Alisema safari za kimataifa zinazofanywa na meli hiyo pia zimeweza kuimarisha uhusiano na kufungua milango kwa sekta nyingine zikiwamo za kibiashara, utalii na utamaduni kati ya Zanzibar na Visiwa vya Comoro, na Kenya.

mwanzo| Habari| Jifunze Kiswahili| Blogu Na Ukumbi| MAKTABANI JISOMEE| picha| video| Makala|