Jinsi arosto inavyowaathiri watumiaji wa dawa za kulevya

Na TUMAINI MSOWAYA

Imepakiwa - Friday, February 17  2017 at  13:16

Kwa Mukhtasari

Daktari bingwa mwandamizi wa Tiba na Afya ya Akili katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Frank Masao amesema mtumiaji aliyeacha ghafla matumizi ya dawa za kulevya hupata tatizo la arosto linalowasumbua sana.

 

DAR ES SALAAM, Tanzania

DAKTARO bingwa mwandamizi wa Tiba na Afya ya Akili katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Frank Masao amesema mtumiaji aliyeacha ghafla matumizi ya dawa za kulevya hupata tatizo la arosto linalowasumbua sana.

Alisema mtumiaji anapokosa kilevi, arosto huwa kali zaidi ya siku tatu za kwanza, hupungua kati ya wiki moja hadi mbili na ili hamu ya matumizi ya dawa za kulevya imalizike kabisa huweza kuchulua hadi miaka miwili.

Hata hivyo, ameshauri kuwa watumiaji wanaaaaoshikiliwa na polisi wanapasa kupewa matibabu kwa sababu dawa za kulevya  zina madhara mmwilini  hapo hawafi isipokuwa wanateseka.
Akizungumza na gazeti hili kkatika mahojiano  maalumu jana, Dkt Masao alisema arosto ni kitendo cha mtumiaji  wa kilevi hutamani  au kuwa na kiu zaidi ya kukitumia kilevi hicho wakati  anapokosa.

Dkt Mmasao alisema arosto ya kila dawa hutofautiana na kwamba mtumiaji wa heroini  anapokosa kilevi hicho, huanza kupiga miayo, hutoa machozi, kamasi, maumivu makali ya viungo, tumbo na kuharisha.

“Pia huwa anaksa hamu ya kula, hapati usingizi, hofo iisiyo na ulazima hatulii sehemu moja, anakosa amani na huwa na hamu ya kilevi hicho kupindukia”, alisema.

Dkt Masao alisema kawaida katika kichwa cha binadamu kuna sehemu inayoitwa “Mesolimbiq System” au “Reward Stystem” ambayo ndiyo huwa inasababisha mtu kuendelea au kuiacha tabia fulani.

Alidai kuwa sehemu hiyo huwa inatoa kemikali inayoitwa “Dopamine”, hivyo ikiwa utatumia daa a kullevya zozote zile huwa zinasababisha kemikali hiyo kutoka na kmfanya mtumiaji ajisikie raha zaidi.

“Kile kitendo cha kujisikia raha maana yake ni kwamba Dopamine imeahiliwa na isiopoachillliiiwa utajisikia kinyume chake. Pia huwa zinaacha kumbukumbu kwenye ubongo na baada ya ya muda raha hiyo ikiisha mtu anatamani kuipata, hivyo ni lazima Dopamine itoke tena.

“Ndiyo maana mtu anayetumia ulevi baada ya muda fulani anakuwa hana ujanja ni lazima atumie tema kilevi kwa sababu “Dippamine” zinakuwa wazi. Ile hamu  kupindukia ndiyoa mabyo tunaita ‘arosto’ na hapo hullazimika kufanya kila kinachowezekana kupata kilevi,” alisema.

Uhalifu

Aliongeza watumiaji wa dawa za kulevya wanapokuwa na arosto hujikuta wakifanya vitendo vya uhalifu ilimradi wapate  fedha za kununua dawa za kulevya kumaliza hamu waliyonayo.

“Ile hamu ya kuvuta kwenye ubongo wake huwa inakaa hai miaka miwili na ndiyo maana sisi wataalamu, yule unamwona ni mgonjwa. Kwa wataalamu mtu huyu kumfunga ni kuendelea kumtesa. Anatakiwa kutibiwa kwa sababu hamu haiishi,” alisema.

Alisema kwa sabbau hamu hamu hiyo huwa inakaa muda mrefu na mtu huyo akitoka ‘sober house’ baada ya muda mfupi na ikiwa hajapata mafunzo stahili ataanza tena matumizi ya dawa za kulevya.

“Kuna baadhi ya ‘sober house’ huwa zinatoa mafunzo stahili kama namna ya kukwepa matumizi ya  dawa hizo, kukwepa marafiki wabaya, kufanya kazi halali,” alisema.

Dkt Masao alisisitiza kuwa kwa kibinadamu huwa wanateseka na kuhtaji tiba.

“Kile kitendo cha kujisikia raha maana yake ni kwamba Dopamine imeachiliwa na isipoachiliwa utajisikia kinyume chake.Pia huwa zinaacha kumbukumbu kwenue ubongo baada ya muda raha hiyo ikiisha mtu anatamani kuipata tena .Hivyo ni lazima ‘Depamine’ itoke tena.”