UCHUMI NA BIASHARA

EABL yapata faida ya Sh4.9 bilioni

Msimamizi Mkuu wa EABL, Bw Seni Adetu.

Picha/MATKABA Msimamizi Mkuu wa kampuni ya East African Breweries Limited, Bw Seni Adetu, akihutubia wanahabari Agosti 26, 2011. 

Na PETER MWAI  ( email Mwandishi)

Imepakiwa - Friday, February 17  2012  at 20:2

Kwa Mukhtasari

Faida hiyo ni ongezeko la asilimia 17 ikilinganishwa na Sh4.2 bilioni iliyopata katika kipindi cha mwaka 2010. Faida kwenye kila hisa iliongezeka Sh4.03 mnamo 2010 hadi Sh5.55.

KAMPUNI ya East African Breweries ilipata faida ya Sh4.9 bilioni katika kipindi cha nusu mwaka kilichomalizika Desemba 31.

Hili ni ongezeko la asilimia 17 ikilinganishwa na Sh4.2 bilioni iliyopata katika kipindi cha mwaka 2010 kwa mujibu wa matokeo ya kifedha yaliyotolewa jana.

Matokeo hayo yametolewa siku moja tu baada ya kustaafu kwa mwenyekiti wa bodi wa muda mrefu, Bw Jeremiah G Kiereini, aliyehudumu kwa miaka 24 tangu mwaka wa 1988.

Amekuwa akihusika sana kwenye kampuni nyingi tangu kuondoka kutoka serikali ya Rais Mstaafu Daniel Moi ambapo alikuwa Katibu Mkuu, 1984.

Mrithi wa Kiereini

Wadhifa wake katika EABL, umechukuliwa na Bw Charles Muchene ambaye alikuwa mshauri mkuu katika kampuni ya PricewaterhouseCoopers.

Faida ya EABL kwenye kila hisa iliongezeka Sh4.03 mnamo 2010 hadi Sh5.55.

Mgao wa faida ambao utalipwa wenye hisa umeongezeka kutoka Sh345 milioni nusu ya mwaka iliyotangulia hadi Sh546 milioni.

Katika kipindi hicho, EABl ilinunua mali na mashini zenye thamani ya Sh3 bilioni, na pia kununua hisa za NCI kwa Sh21 bilioni.

 

Most Popular

Wabunge 175 kutahiriwa Zimbabwe

Wabunge 175 nchini Zimbabwe watapashwa tohara kufikia mwisho wa mwezi ujao katika juhudi za kuhamasisha wanaume

Mwanawe Waziri wa Fedha ajitia kitanzi

MWANAWE Waziri wa Fedha Njeru Githae anadaiwa kujiua nyumbani kwao Runda, Nairobi. Polisi wameanzisha uchunguzi

Polisi waendelea kusaka walioshambulia Mombasa

Polisi wameanzisha msako mkali kutafuta washukiwa waliotekeleza shambulio la kigaidi katika mkahawa wa Bella Vista,

Utengano wakumba ukumbusho wa Wanjiru

Ibada mbili tofauti zilifanywa kuadhimisha mwaka mmoja tangu kifo cha bingwa wa marathon katika Olimpiki Samuel