KQ yazindua ndege mpya ya kubeba mizigo

Msimamizi Mkuu wa Kenya Airways Titus Naikuni

Picha/DIANA NGILA Msimamizi Mkuu wa shirika la ndege la Kenya, Dkt Titus Naikuni, wakati wa uzinduzi rasmi wa ndege aina ya Boeing 747-400F katika uwanja wa ndege wa JKIA, Februari 21, 2012. 

Na MILKAH RIGHA  ( email Mwandishi)

Imepakiwa - Wednesday, February 22  2012  at 19:3

Kwa Mukhtasari

Ndege hiyo, iliyozinduliwa na Kampuni ya ndege ya Kenya Airways (KQ)  kwa ushirikiano na kampuni ya KLM Royal Dutch, mnamo Jumanne, itakuwa ya kwanza kabisa  itakayotoka Uchina moja kwa moja hadi Afrika.

 

WAFANYIBIASHARA wa Kenya wataweza kusafirisha jumla ya tani 120 za bidhaa zao kwa wakati mmoja, kufuatia kuzinduliwa kwa ndege  mpya ya mizigo nchini.

Ndege hiyo, iliyozinduliwa na Kampuni ya ndege ya Kenya Airways (KQ)  kwa ushirikiano na kampuni ya KLM Royal Dutch, mnamo Jumanne, itakuwa ya kwanza kabisa  itakayotoka  Uchina moja kwa moja hadi Afrika.

Huduma za ndege hiyo ya mizigo aina ya Boeing 747-400F, inayomilikiwa na shirika la Martin Air, ambalo ni sehemu ya shirika la ndege la Air France KLM, zitatolewa na KQ kwa ushirikiano  na KLM Cargo.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi, Mkurugenzi Mkuu wa Kenya Airways, Bw Titus Naikuni, alisema kwamba kampuni hiyo inanuia kununua ndege nyingine mbili,  katika kipindi cha pili cha mwaka huu. Aliongeza kwamba zitasaidia pakubwa kufungua nafasi za kazi kwa watu wengi nchini.

“Tunatarajia ndege nyingine 12 kama hizi katika kipindi cha miaka 10 ijayo, na tuna hakika kwamba hiyo itasaidia kubuni nafasi za kazi na kupunguza idadi ya vijana wasio na ajira,” alisema Bw Naikuni.

Aidha aliongeza kwamba, Kenya itasafirisha maua na chakula hadi Uchina kupitia kwa huduma hii huku ikipokea vifaa vya kielektroniki, vipuri vya mashine, simu na bidhaa nyingine kutoka Uchina.

Bidhaa za ujenzi zitasafirishwa kutoka  Amsterdam hadi Uchina.  Aidha inalenga kusaidia  katika kukua kwa uchumi wa Kenya na mataifa mengine ya Afrika, na pia kupunguza kutegemea sehemu ya mizigo ya ndege za kawaida za abiria, ambazo zimekuwa zikitegemewa licha ya uwezo wake mdodo wa kubeba mizigo.

“Biashara baina ya Uchina na Kenya inazidi kupanuka, hivyo ndege hii itasaidia sana kuimarisha uhusiano mkuu kati ya nchi hizi mbili,” alisema Meneja wa Mizigo wa Kampuni ya Martinair Cargo, Camiel Eurlings.

Ndege hiyo inatarajiwa kuhudumu kati ya Amsterdam-Guangzhou (Uchina)- Nairobi na kurudi Amsterdam.

Vilevile, inatarajiwa kufanya safari zake kutoka Nairobi kupitia mji wa Lagos, Nigeriac kabla ya kuenda katikia Uwanja wa Ndege wa  Amsterdam, Uholanzi, kuanzia Mei mwaka huu.

Ndege hii itafanya safari mbili kamilifu kati ya miji hii mitatu kwa wiki.

Kwa sasa, huduma ya mizigo ya KQ imekuwa ikiletea shirika hili jumla ya asilimia 8-9 ya mapato yake na inatarajiwa kuongeza  mapato haya hadi asilimia 15, katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Share Bookmark Print

Rating

 

 

 

 

 

 

Most Popular

Wabunge 175 kutahiriwa Zimbabwe

Wabunge 175 nchini Zimbabwe watapashwa tohara kufikia mwisho wa mwezi ujao katika juhudi za kuhamasisha wanaume

Mwanawe Waziri wa Fedha ajitia kitanzi

MWANAWE Waziri wa Fedha Njeru Githae anadaiwa kujiua nyumbani kwao Runda, Nairobi. Polisi wameanzisha uchunguzi

Polisi waendelea kusaka walioshambulia Mombasa

Polisi wameanzisha msako mkali kutafuta washukiwa waliotekeleza shambulio la kigaidi katika mkahawa wa Bella Vista,

Utengano wakumba ukumbusho wa Wanjiru

Ibada mbili tofauti zilifanywa kuadhimisha mwaka mmoja tangu kifo cha bingwa wa marathon katika Olimpiki Samuel