Uingizaji wa bidhaa kutoka Kenya waporomoka

Namanga

Barabara ya kuenda kwa ofisi za idara ya uhamiaji mjini Namanga; mpakani Kenya na Tanzania palitokea maandamano Wakenya wakidai wanahangaishwa na maafisa wa Tanzania Machi 27, 2016. Picha/JOSEPH NGUNJIRI 

Na MWANDISHI WETU

Imepakiwa - Wednesday, August 9  2017 at  10:24

Kwa Mukhtasari

Usafirishaji wa fedha za Kenya kuja Tanzania umeporomoka kwa asilimia 34 ikilinganishwa na Ksh12.55 sawa na Sh251 bilioni zilizorekodiwa katika kipindi kama hicho mwaka 2016 katika kipindi cha miezi mitano ikiwa ni kiashiria cha matokeo hasi ya vizuizi vilivyowekwa kwenye biashara.

 

DAR ES SALAAM, Tanzania

USAFIRISHAJI wa fedha za Kenya kuja Tanzania umeporomoka kwa asilimia 34 ikilinganishwa na Ksh12.55 sawa na Sh251 bilioni zilizorekodiwa katika kipindi kama hicho mwaka 2016 katika kipindi cha miezi mitano ikiwa ni kiashiria cha matokeo hasi ya vizuizi vilivyowekwa kwenye biashara.

Biashara imeporomoka kwa kiasi cha Ksh 4.5bilioni (sawa na Tsh87 bilioni) hadi Ksh 8.2 (Tsh164 bilioni) mpaka kufikia Mei mwaka huu, ikilinganishwa na Ksh12.55 bilioni (Tsh 251 bilioni) zilizorekodiwa katika kipindi hicho mwaka 2016.

Kwa muijibu wa takwimu zilizotolewa na Ofisi ya Takwimu ya Kenya (KNBS) usafirishaji wa bidhaa kwenda Uganda imeendelea kukua na kuimarisha nchi hiyo katika bidhaa zinazozalishwa viwandani.

Kwa upande mwingine Tanzania imekuwa kwenye mgogoro wa muda mrefu wa kufikia masoko ya Kenya mgogoro ulioongezeka zaidi mwezi Mei baada ya Tume ya Udhibiti wa Nishati ya Kenya kupiga marufuku kuingiza kwa gesi nchini humo kupitia mpaka wa Namanga kwa kile walichodai ni sababu za ubora.

"Tanzania imekuwa ikiuza gesi ya LPG kwa zaidi ya miaka kumi. Biashara hii imeimarika sana. Tumewekeza na tunazidi kuwekeza kwenye miundombinu ili kuhakikisha kwamba tunaimarisha soko la pamoja la Afrika Mashariki,” imesomeka sehemu ya taarifa ya wafanyabiashara wa Tanzania.

Hata hivyo, Tanzania ilijibu mapigo kwa kuzuia uingizwaji wa maziwa na sigara kutoka Kenya.