http://www.swahilihub.com/image/view/-/4740936/medRes/2097671/-/11k250g/-/mdaresa.jpg

 

Vitambulisho vyawachongea Wamachinga

Paul Makonda

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Picha/MAKTABA 

Na MOSENDA JACOB, Mwananchi

Imepakiwa - Wednesday, January 30  2019 at  11:50

Kwa Muhtasari

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutoa hadi Machi mosi kila machinga awe na kitambulisho maalumu.

 

DAR ES SALAAM, Tanzania

KUTOLEWA kwa vitambulisho maalumu vya wamachinga huenda ukawa mwanzo wa wengine kuondoka katika sekta hiyo, baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutoa hadi Machi mosi kila machinga awe na kitambulisho hicho vinginevyo atatakiwa kuonyesha leseni ya manispaa na vibali vya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Pia, amewapa miezi miwili watendaji wa mkoa huo, wakuu wa wilaya na watendaji kata kuhakikisha wanaweka taarifa za vitambulisho vya wamachinga katika kanzidata moja.

Makonda alitoa maagizo hayo Jumanne wakati wa mkutano wake na watendaji wa mkoa ikiwa ni siku moja baada ya Rais John Magufuli kuwapatia vitambulisho vingine wakuu wote wa mikoa ambavyo wamachinga watavipata kwa kulipia TSh20,000.

Alisema ikifika Machi mosi machinga ambaye atakuwa hana kitambulisho hicho atapaswa kuonyesha leseni zake za biashara za TRA la sivyo hatua kali zitachukuliwa.

“Takwimu za pamoja zitasaidia kufuatilia mwenendo wa kila machinga ndani ya mkoa wetu na kurahisisha mchakato wa kutoa vingine ifikapo 2020, hivyo basi nawapa muda hadi Machi 29 muwe mmemaliza.”

Alisema kwa awamu ya kwanza Dar es Salaam ilipewa vitambulisho 25,000, awamu ya pili 25,000 na awamu ya tatu 75,000 ambavyo vyote vimetolewa kwa wamachinga.

50,000 ambavyo tumevipokea Jumatatu (juzi) tutavigawa kwa wahusika haraka.