http://www.swahilihub.com/image/view/-/3095820/medRes/1267449/-/11esyewz/-/TFWemaSepetu1.jpg

 

Wakali kinoma, ila wametoswa

Wema Sepetu

Mwigizaji wa Filamu za Bongo Wema Sepetu. Picha/HISANI 

Na RHOBI CHACHA

Imepakiwa - Friday, May 11  2018 at  13:53

Kwa Muhtasari

Wakati mapenzi yakiwa moto basi lazima dunia ijue.

 

HAKUNA raha kama kupendwa Wakati mapenzi yakiwa moto basi lazima dunia ijue.

Ndiyo unakumbuka wakati penzi la staa wa Bongo Flava, Diamond na malkia wa Bongo Movie, Wema Sepetu mambo yalikuwa ni moto.

Mitandao yote ya kijamii ilikuwa inapambwa na picha za malovee za Wema na Diamond na hata walipoamua kupigana chini bado uhusiano huo uliendelea kutrend kwenye mitandao mpaka sasa unaendelea kutamba.

Lakini, sio Diamond na Wema tu kwani, hata mastaa wengine wamekuwa wakiyaweka mahusiano yao hadharani na kujitangaza kwenye mitandao ila mambo yanapoharibika balaa huanzia hapo.

Mwanaspoti linakuletea baadhi ya mastaa wa kike wenye majina makubwa Bongo ambao licha ya kuwa warembo, lakini wamejikuta wakiteswa na mapenzi na kubaki kulialia kila kukicha.

Wema Sepetu

Mbali na kuwa malkia wa Bongo Movie, Wema ambaye pia ni Miss Tanzania mwaka 2016, alisumbua sana wakati akitoka kimapenzi na Idris Sultan na Kanumba kiasi hata watoto wadogo kuufahamu. Lakini, bahati mbaya kwake amekuwa akishindwa kudumu kwenye mahusiano kwa muda mrefu licha ya kuwa na sura nzuri, sauti tamu na shepu ndio usiseme.

Wema pengine ndiye staa mwenye kujua hasa maumivu ya mapenzi kwa sababu mara nyingi hushindwa kuendelea na mapenzi kutokana na kutendwa hivyo, kubaki na maumivu.

Kuna wakati Wema aliweka bayana kwamba, ameumizwa sana hivyo hataki tena kuingia kwenye mapenzi na wanaume ambao hajatumia muda mrefu kuwachunguza.

Akizungumza na Mwanaspoti, Wema alisema upendo wa kweli anaounyesha katika mapenzi ndio umekuwa silaha ya kumuumiza na kumwacha na maumivu.

“Nadhani kujiweka wazi kwangu katika mapenzi na kuwa na upendo wa dhati kwa mpenzi wangu ndio sababu ya kuumizwa, maana nina ugonjwa wa kupenda huwa sinaga maigizo katika mapenzi,” alisema Wema.

Huyu hapa sasa Wolper mwenyewe, ambaye naye amekuwa akipitia misukosuko mingi katika mapenzi. Kama wewe ni mwanaume wa kweli huwezi kumuangalia Wolper na kumuacha apite tu bila kurusha neno au kukodoa macho kwani, amekamilika idara zote unaambiwa.

Hata hivyo, ameshakutana na visanga kibao vya mapenzi ikiwemo kuvishwa pete za uchumba kisha wanaume haooo wanasepa zao mdogo mdogo na kumuacha kwenye majonzi.

Wolper ameliambia Mwanaspoti kuwa, kinachomsababisha kutendwa na kuumizwa katika mapenzi, ni kile tabia yake ya kutopenda kufanya siri mahusiano yake ya kimapenzi pamoja na kumpenda sana mwanaume wake.

“Unajua sina mapenzi ya siri, napenda nikiwa na mwanaume ni huru na nimuonyeshe hadharani kuwa nampenda sana, ndio maana huwa wananiumuza sababu wanajua nawapenda.

Napenda kujiachia na kumfanyia mpenzi wangu kila anachotaka kinapokuwa ndani ya uwezo wangu, lakini mwisho wa siku mapenzi hugeuka shubiri,” amefunguka Wolper.

Kajala Masanja

Staa huyu ni mrembo lakini na yeye ameonja maumivu makali ya mapenzi kutokana na kuumizwa mara kwa mara katika mapenzi.

Kajala naye alishawahi kusema mapenzi basi kutokana na kulizwa na mwanamume anayempenda.

Huyu ni mwanamke ambaye ana historia ya kusisimua katika chungu na tamu ya mapenzi na hata kwenye ndoa kwani, ameshaionja ndoa na yakamshinda vilevile.

Hamisa Mobeto

Ni mrembo, mama wa watoto wa wawili ambapo mwanaye wa kwanza alizalishwa na bosi mkubwa wa EFM, lakini wakaja kumwagana mchana kweupee.

Hivi karibuni mrembo huyo ameingia kwenye vichwa vya habari baada ya kuripotiwa kuzaa na Diamond, lakini uhusiano wao licha ya kupata naye mtoto ukaishia kuwa mchungu.

Mbaya zaidi tayari walikuwa na mtoto hivyo, wakalazimika kufikisha kwenye vyombo vya sheria kudai matunzo, lakini ishu ya karibu kuhusiana na wazazi hawa wawili ndio kama mlivyosikia na kuona huko mitandaoni.

“Mimi ni mwanamke mvumilivu sana katika mapenzi, sio mhangaikaji sana wa mapenzi na ndio maana hata nikitendwa naumia, lakini narudi kukaa chini kujifikiria na naendelea na mambo mengine ya maisha,” alilifungukia Mwanaspoti.