Wasichana 400 waliopata mimba shuleni wakumbukwa

Na SADA AMIR

Imepakiwa - Wednesday, June 13  2018 at  15:04

Kwa Muhtasari

Matumaini ya wasichana waliokatisha masomo kwa kupata mimba Mikoa ya Kanda ya Ziwa yameanza kurejea, baada ya shirika la Education for Better Living Organization (EBLI) la jijini Mwanza kuwaanzishia programu maalumu ya ujasiriamali.

 

MWANZA, Tanzania

MATUMAINI ya wasichana waliokatisha masomo kwa kupata mimba Mikoa ya Kanda ya Ziwa yameanza kurejea, baada ya shirika la Education for Better Living Organization (EBLI) la jijini Mwanza kuwaanzishia programu maalumu ya ujasiriamali.

Tayari programu hiyo imenufaisha zaidi ya wasichana 600 ambao wamesomea ujasirimali, utaalamu wa kompyuta, uhazili na urembo.

Akizungumza jijini Mwanza juzi, mkurugenzi wa EBLI, Bernard Makachia alisema kati ya wahitimu hao, 400 ni wasichana waliokatisha masomo kwa kupata mimba na waliosalia ni walioacha shule kwa sababu zingine ikiwamo kukosa ada, utoro au kwenda mijini kufanya kazi za nyumbani.

Naye meneja miradi wa EBLI, Andrew Mwakibolwa, alisema programu hiyo pia inawahusisha wavulana waliokatisha masomo kwa sababu mbalimbali.