http://www.swahilihub.com/image/view/-/4703552/medRes/2073062/-/m89wm3/-/sdad.jpg

 

‘Watendaji nendeni kwa wananchi’

Dkt Abdulla Juma Saadalla

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt Abdallah Juma Saadalla maarufu kama Mabodi. Picha/MAKTABA 

Na HAJI MTUMWA, Mwananchi

Imepakiwa - Friday, December 7  2018 at  13:04

Kwa Muhtasari

Dkt Abdallah Juma Sadallah ‘Mabodi’ anaamini ziara za kiutendaji za watendaji wa serikali za mitaa kwa wananchi wa ngazi za chini zitatafutia ufumbuzi wa kudumu changamoto zinazowakabili.

 

hmtumwa@mwananchi.co.tz

UNGUJA, Tanzania

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt Abdallah Juma Sadallah ‘Mabodi’ amewataka watendaji wa Serikali za mitaa Zanzibar kujenga utamaduni wa kufanya ziara za kiutendaji kwa wananchi wa ngazi za chini ili kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu changamoto zinazowakabili.

Mabodi alitoa wito huo akiwa katika ziara zake za kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM katika halmashauri ya wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja jana.

“Ni lazima watendaji na viongozi washuke kwa wananchi kufuatilia masuala mbalimbali yatakayosaidia kumaliza changamoto zinazowakabili katika ngazi za Serikali za mitaa,” alisema.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM, mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo, Mussa Ali Makame alisema katika ukusanyaji wa mapato mwaka 2018/2019 wamekisia kukusanya TSh869.3 milioni na hadi Novemba walikusanya TSh157.6 milioni sawa na asilimia 18.