Na JOSEPH LYIMO

Imepakiwa - Friday, November 9  2018 at  13:07

Kwa Muhtasari

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Tumaini Magesa amesema kiongozi au mtumishi atakayeshindwa kulima kitaalamu ili wakulima wajifunze kutoka kwake, atakuwa halali yake.

 

KITETO, Tanzania

MKUU wa Wilaya ya Kiteto, Tumaini Magesa amewataka watumishi na viongozi wa kisiasa wanaojihusisha na kilimo, kulima kitaalamu; vinginevyo ataagiza polisi wawasweke rumande.

Magesa alisema hayo juzi akizungumza kwenye Baraza la Madiwani wa Halmashauri.

Alisema kiongozi au mtumishi atakayeshindwa kulima kitaalamu ili wakulima wajifunze kutoka kwake, atakuwa halali yake.

“Nitatembelea mashamba ya watumishi na madiwani ambayo yatakuwa mfano, nikukute umelima kienyeji,” alisema Magesa.

Naye mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Lairumbe Mollel alimuomba kuwageukia pia wafugaji wafuge kisasa.