Isimu pamoja na matawi mbalimbali ya Isimu katika Kiswahili

Na MARY WANGARI

Imepakiwa - Monday, December 3  2018 at  06:43

Kwa Muhtasari

Elizabeth Nagemi aliuliza swali akitaka kujua matawi ya semantiki na uhusiano kati ya semantiki na matawi mengine ya kiisimu.

 

JINA: Elizabeth Nagemi

Swali: Hujambo? Tafadhali nieleze matawi ya semantiki na uhusiano kati ya semantiki na matawi mengine ya kiisimu

Katika makala ya leo, tutaanza uchambuzi kuhusu Isimu ikiwemo matawi mbalimbali ya isimu katika Kiswahili.

Isimu ni nini?

Isimu ni taaluma ya Kisayansi inayojishughulisha na maswala ya lugha. Kuna mambo kadha wa kadha yanayoifanya isimu kutambuliwa kama somo la Sayansi.

Sifa za Isimu kama Sayansi

Matumizi ya Hesabu

Kuna matumizi ye hesabu wakati tunapoongea kuhusu asilimia. Hesabu bila shaka ni somo la Kisayansi na huitwa takwimu leksika (lexico statistics).

 

Biolojia/ Elimu Viumbe

Kipengele hiki huchunguza maneno kutoka kinywani na vile yanavyotoka pamoja na yanakotoka. Biolojia pia ni somo mojawapo la Sayansi

 

Maabara ya lugha

Maabara hutumika katika kufanya uchunguzi wa lugha hasa katika nchi zilizoendelea sana kama vile Marekani, Ujapani, Ujerumani, Uingereza, Ufaransa na nyinginezo. Kazi inayohusiana na maabara bila shaka ni ya Kisayansi.

 

Isimu hutumia mbinu za Kisayansi katika matumizi yake. Inahusu uwaziu naotokana na jinsi maneno yalivyopangwa ili kuleta maana iliyo wazi na wala sio kiholelaholela. Katika isimu kuna matumizi ya nguvu katika matamshi ya maneno.

 

Matumizi ya Fizikia

Fizikia ni somo la kisayansi ambalo hujihusisha na matumizi ya nguvu yoyote ile, ikiwemo nguvu za binadamu, mnyama, jua, nyuklia.

 

Ukosefu wa hisia za kibinafsi

Isimu Pendekezi (prescriptive linguistics) inapendekeza; kwa mfano, katika lugha mama. Isimu Elekezi (descriptive linguistics) hasa hutokea tuapotumia lugha ya pili.

 

Isimu imegawanywa katika makundi mawili:

 

1. ISIMU PWEKE

Tawi hili linajishughulisha na jinsi sauti za lugha zinavyotamkwa.Isimu hii nayo ina matawi madogo kama vile:

 i.                         fonetiki

 ii.                         fonolojia

 iii.                        mofolojia

 iv.             sintaksia

 v.             semantiki

vi. pragmatiki

2. ISIMU TUMIZI

Tawi hili pia limegawika katika makundi madogo madogo kama vile:

 

i.            isimu saikolojia

ii.            isimu historia

iii.           isimujamii.

 

Isimu jamii (Social-linguistics)

Ni tawi la isimu (elimu ya lugha) linalochunguza namna lugha inavyotumika katika jamii na uhusiano baina yake.

Tawi hili huchunguza matumizi ya lugha katika mazingira tofauti, aina mbalimbali za lugha na mazingira yake, uhusiano kati ya lugha na utamaduni wa jamii inayoitumia.

Marejeo:

Mbaabu, I., (1996). Language Policy in East Africa: A Dependency Theory Perspective. Nairobi: Educational Research and Publications.

Masebo, J.A., Nyangwine A. D., (2002) Nadharia ya Lugha: Kiswahili 1. Dar es Salaam: Afroplus Industries Ltd.

Massamba, D.P.B., (2002) Historia ya Kiswahili 50 BK., Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.

Ipara, I. O., Waititu, F.G., (2006). Ijaribu na Uikarabati. Nairobi: Oxford University Presss.

Habwe, J., (2006). Darubini ya Kiswahili. Nairobi: Phoenix Publishers.