Kushughulikia maswali kutoka kwa wasomaji wetu

Na MARY WANGARI

Imepakiwa - Tuesday, November 13  2018 at  12:44

Kwa Muhtasari

Msomaji wetu Mutunga Ndeto anasema amekuwa akifuatilia makala za mwandishi na angependa kuomba atumiwe maandishi kuhusu aina nne kuu za uandishi.

 

NACHUKUA fursa hii kuwashukuru na kuwapongeza wasomaji wetu ambao wamekuwa wakifuatilia na kusoma makala zetu za kujielimisha zaidi kuhusu lugha yetu ya Kiswahili.

Nimekuwa nikipokea maswali mengi kutoka kwa wasomaji wetu wakiomba niangazie mada fulani huku wengine wakitaka uchambuzi wa kina kuhusu mada nilizoshughulikia awali.

Kwa mintarafu hiyo, nitakuwa nikiangazia mada hizo kwa kuanza na maswali niliyopokea awali hadi ya hivi karibuni na ninatumai hatua hii itawaridhisha na kuwanufaisha wasomaji wetu huku tukizidi kujifahamisha mengi katika ukumbi wa lugha.

Nawashukuru nyote.

Tunaanza na swali kutoka kwa msomaji wetu Mutunga Ndeto.

SWALI

Nimekuwa nikifuatilia makala zako na ningependa kuomba unitumie maandishi kuhusu aina nne kuu za uandishi.
Asante

UANDISHI

Dhana ya uandishi inaweza kufafanuliwa kama mbinu au njia ya mawasiliano kati ya watu inayowakilisha lugha na hisia kwa alama na ishara zilizorekodiwa.

Uandishi katika lugha nyingi hukamilisha mawasiliano ya sauti ukitumia miundo yake mathalani maneno, sarufi na semantiki.

Kando na kuwa lugha, uandishi pia ni aina ya teknolojia iliyostawi pamoja na vifaa vinavyotumika miongoni mwa wanajamii.

Matini – ni matokeo au kinachopatikana kwa kutokana na uandishi.

Msomaji – ni anayelengwa na mwandishi au anayepokea kazi ya mwandishi

Baadhi ya sababu za kuandika ni pamoja na kwa madhumuni ya kutoa vitabu, uandishi wa shajara hadithi na kadhalika.

Manufaa ya uandishi yanajitokeza katika mambo yafuatayo:

  1. Kudumisha na kuhifadhi utamaduni
  2. Kuhifadhi kumbukumbu za historia
  3. Kusambaza ujuzi na maarifa
  4. Kuunda mifumo ya sheria
  5. Huwezesha pia watunzi kutoa kazi zao kama vile washairi na watunzi wengine.

Sanaa ya uandishi imezidi kukua na kubadilika kadri na mpito wa wakati na jinsi jamii inavyozidi kukua na maendeleo ya sayansi na teknolojia katika jamii.

Baadhi ya matukio yaliyoshinikiza mabadiliko ya maandishi katika jamii kihistoria ni kama vile maendeleo ya biashara na utawala huko Mesopotamia katika Karne ya 4 KK, Misri ya Kale na Amerika ya Kati ambayo yalizidi uwezo wa kumbukumbu ya binadamu na kuhitaji kuhifadhiwa katika maandishi.

 

Falkenstein, A. 1965 Zu den Tafeln aus Tartaria. Germania 43, 269–273

Maxim, Z. 1997 Neo-eneoliticul din Transilvania. Bibliotheca Musei Napocensis 19. Cluj-Napoca

Paul, I. 1995 Vorgeschichtliche untersuchungen in Siebenburgen. Alba Iulia

Vlassa, N. 1965 --- (Atti UISPP, Roma 1965), 267–269